DAR ES SALAAM: POLISI WAMWAGWA MITAANI

DAR ES SALAAM: POLISI WAMWAGWA MITAANI

Wakuu, Leo katika pitapita zangu maeneo ya Morroco nimekutana na gari za polisi za kutosha wakiwa wamevalia special kupambana na waandamanaji samba samba na hilo pia gari za maji ya kuwasha zlikua znapita pita maeneo hayo
Wanapambana nao kwani kuna mashindano? Hayo maandamano ni ya Amani, labda wanalinda waandamanaji..
 
Kwani lazima iwe Dar? Sisi tutaandamana huku kizi zege halilali
Mimi naandamana huku kiembe mbuzi .....nakaa jirani na nyumba ya balozi. Kwa hiyo nitaandamana kwenda kwa balozi wa mtaa anakaa nyumba ya tatu kutoka kwangu navuka nyumba moja tu nampelekea malalamiko haiwezekani tudakwe kama kuku bandani
 
Wakuu, Leo katika pitapita zangu maeneo ya Morroco nimekutana na gari za polisi za kutosha wakiwa wamevalia special kupambana na waandamanaji samba samba na hilo pia gari za maji ya kuwasha zlikua znapita pita maeneo hayo
Ndio mazungumzo anayosema Samia anafanya na vyama vya upinzani.
 
Hata mimi nimewaona maeneo ya Tabata Matumbi kielekea Daraja la Buguruni
Asubuhi nimekutana nao mataa ya Changombe-wamejazana kwenye gari tano maana nilizihesabu wakielekea maeneo ya uwanja wa taifa, mchana nimepishana nao wakiwa kundi soko la Karume wakitembea kwa miguu wakielekea Kariakoo.
 
Hii ni kweli kuna mwanangu yupo dodoma kikazi kaniambia amekosa chupuchupu kwenda dar kula per diem za kuzuia maandamano.
nchi yetu kwa sasa ina askari wachache sana.ndio maana wanaogopa kusiwe na maandamano.kwasababu watalazimika kuomba askari kutoka mikoa mingine. huko wanakoomba askari usalama wa huko utakuwaje. na hawa wanaoitisha maandamano wanalijua hili wanawachokoza makusudi.kwa kifupi wanaisumbua serikali sana. lakini pamoja na kuisumbua serikali .serikali haipaswi kuwaumiza ni haki yao.
 
Back
Top Bottom