Dar es Salaam: Polisi waua majambazi wanne na kufanikiwa kukamata silaha mbalimbali

Dar es Salaam: Polisi waua majambazi wanne na kufanikiwa kukamata silaha mbalimbali

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WANNE NA KUPATIKANA BASTOLA MOJA, RISASI MOJA, MAGANDA MANNE YA RISASI NA MILIPUKO MIWILI YA KUTENGENEZA KIENYEJI.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam mnamo tarehe 15.08.2020 majira ya saa tisa na nusu alasiri kupitia kikosi kazi chake kimefanikiwa kuwaua majambazi sugu wanne na kufanikiwa kukamata silaha moja bastola aina ya Bereta iliyofutwa namba zake za usajili ikiwa na risasi moja ndani ya magazine na maganda manne ya risasi, tochi moja na milipuko miwili ya kutengeneza kienyeji.

Katika tukio hilo awali alikamatwa mtuhumiwa aitwaye NURU THADEI miaka 34, mkazi wa Kinyerezi kwa mahojiano ya matukio mbalimbali ya uhalifu, ndipo alikiri kuwa alikuwa gerezani kwa kesi ya mauaji ya Mchina maeneo ya kurasini mwaka 2011 kesi PI No.19/2011 na aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 2017 na kuunda genge la wahalifu na wenzake wengine walioachiwa gerezani.

Aidha jambazi huyo aliwaongoza askari kwenda kuwaonyesha walipo majambazi wengine na kuonyesha silaha wanazomiliki ndipo alipofika eneo la nyumba hiyo wanayoishi na kupanga mipango ya ujambazi alipiga kelele ndipo wale watuhumiwa wengine walianza kurusha risasi kuwaelekea askari, ndipo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi hao, NURU THADEI na wenzake GODFREY FAUSTINE, ANTONY@MNYAMONGO NA PETER SEBA ambao walipofikishwa hospitali waligundulika kuwa wamefariki dunia.

Pia majambazi hao walikuwa na kesi za unyang’anyi wa kutumia silaha maeneo mbalimbali ya jiji.

Baada upekuzi katika nyumba waliyokuwa wakiishi majambazi hao zilipatikana Pesa Tsh 600,000/=, simu za mkononi 5 aina mbalimbali, Laptop moja, Pete za ndoa, mabegi matatu na nguo ambazo ziliibiwa katika matukio ya uporaji ambazo zilihifadhiwa katika nyumba hiyo.

Sambamba na hilo wahanga wa matukio hayo walitambua mali zao zilizoibiwa na miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya utambuzi.


1597748338393.png

1597748525476.png

 
Sasa mbona Nuru naye wamemuua wakati ndie aliyewapeleka kuwaona wengine, maana yake walikuwa naye kwenye gari au alikuwa chini ya ulinzi wao
 

Hizi taarifa za polisi za kuua majambazi siku hizi siziamini tena, na wala msiwe mnaziamini kirahisi. Polisi wetu ni wauaji makatili wa kuogopwa zaidi ya ukoma. Ukweli siwaamini Polisi wetu hata kidogo. Mara nyingine wanaua watu wanasingizia majambazi. Wanazo silaha tele huko vituoni na maganda ya risasi, wanayaweka eneo walilotupa maiti za watu waliowaua halafu wanasema majambazi wameuwawa katika mapambano makali!

Mara ngapi umesikia kuwa polisi ameuwawa katika haya mapambano makali? Ikiwa Kigoma wananchi waliweza kuua polisi wawili kwa silaha za jadi katika mpambano kati ya polisi na wananchi, iweje siku zote majambazi walio na silaha za moto wanashindwa kuua angalau polisi mmoja, au hata kujeruhi askari kwa risasi? Kwamba hao majambazi wanaambiwa nyie pigeni risasi hewani wakati sisi tukiwatwanga risasi?

Tatizo Tanzania hatuna chombo cha kuchunguza taarifa hizi magumeshi. Wanalosema polisi ndio kauli ya mwisho. Ndio, polisi wanasaidia usalama wa raia kwa kiasi fulani, lakini watu wa ovyo sana hawa hapa nchini. NI polisi wachache sana walio waaminifu, na wapo ambao wanachukizwa sana na haya matendo maovu ya wenzao.

Tatizo Tanzania wengi wetu ni malofa wa kudanganywa kirahisi sana na kumeza tu uongo tunaopewa. I hate these liars.
 
Sawa, point yangu ni kuwa walienda naye, na wao walikuwa wanarushiwa risasi kutoka na waliokuwa ndani, how comes waliyekuwa naye kwenye, say usafiri wao naye afe ikiwa wamejibizana na waliokuwa ndani?
Ukute walimpeleka akiwa amefungwa pingu, sasa sijui aliwatoroka akajiunga na wenzake au alipigwa risasi na wenzake wakati wa mapambano.
 
Sawa, point yangu ni kuwa walienda naye, na wao walikuwa wanarushiwa risasi kutoka na waliokuwa ndani, how comes waliyekuwa naye kwenye, say usafiri wao naye afe ikiwa wamejibizana na waliokuwa ndani?
Hapo kuna mchezo mchafu, taarifa za mapolisi huwa ZIMEPINDAPINDA SANA. Ukifuatilia sana unaweza kuta ni kama ule mchezo wa KAMANDA ZOMBE na wale Wafanyabiashara wa madini.

Hata hivyo jambo jema ni kwamba KILA NAFSI ITAONJA MAUTI, sisi sote tu wasafir hapa duniani.

MITANO YA UTAWALA WA MKONO WA CHUMA, INATOSHA....
 
NURU alikamatwa na kuhojiwa na kuwapeleka askari katika nyumba kwa upekuzi.


[emoji1][emoji1]ina maana katika list aliyotaja NURU kuna utata ndania yake kisha wakam....
 
Ukute walimpeleka akiwa amefungwa pingu, sasa sijui aliwatoroka akajiunga na wenzake au alipigwa risasi na wenzake wakati wa mapambano.
Uwezo wa kutumia akili wa mapolisi ni mdogo sana, wanadhani wote tunalingana nao. Mauaji mengi ya KIFEDHULI bado yanafanyika nchini, kilichobadilika mbinu za kuua tu.

ITOSHE TU KUSEMA, UTAWALA HUU WA MKONO WA CHUMA SASA BASI.
 
Kazi nzuri sana hiyo pongezi kwenu, siku hizi hatusikii wezi wakikimbizwa mitaani na wananchi kama zamani, wala majambazi wakifikishwa mahakamani adabu inarudi . Ila tuu msibambikizie watu kesi za ujambazi ueni majambazi ya ukweli tuu. Majambazi na Yafe kabisa.
 
Back
Top Bottom