Dar es Salaam: Rais Magufuli amemsimamisha kazi kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Rais John Magufuli amemsimamisha kazi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao na mkuu wa upelelezi mkoani humo, John Rwamulema kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Novemba 23, 2019 na msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime inaeleza kuwa wawili hao wamesimamishwa kazi wakidaiwa kushirikiana na wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha Canon cha mkoani Shinyanga kukwepa kodi.

“Sababu ya pili ni utovu wa nidhamu kwa kushindwa kutekeleza maelekezo waliyopewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa Mkoa huo, Zainab Telack,” inaeleza taarifa hiyo.
 
Haya matamko ya usiku kucha nayo ni shida...mkuu atakuwa yupo ndotoni aisee.
 
Wawakamate wawanyonge, tuna jeshi LA Polisi katili sana sijawahi kuona maisha yangu yote. Vile viaskari pale Njombe vichukuliwe hatua pia, vina lugha chafu sana sana na vinajifanya vijuaji sana sana
 
Siku hizi wananchi wala haawashtuki wakisikia habari kama hii
 
Wawakamate wawanyonge, tuna jeshi LA Polisi katili sana sijawahi kuona maisha yangu yote. Vile viaskari pale Njombe vichukuliwe hatua pia, vina lugha chafu sana sana na vinajifanya vijuaji sana sana
Njombe sehemu gani??
 
Hao waliotolewa lazima watakuwa walisita pahala kuishighulikia chadema. Hoja zilizotolewa ni kifunika komba,.....
.
 
Na manager wa TRA nae alisita kuishughulikia chadema?

Watanzania tunachanganya siasa na utendaji.
 
Rais John Magufuli amemsimamisha kazi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao na mkuu wa upelelezi mkoani humo, John Rwamulema kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Novemba 23, 2019 na msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime inaeleza kuwa wawili hao wamesimamishwa kazi wakidaiwa kushirikiana na wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha Canon cha mkoani Shinyanga kukwepa kodi.

“Sababu ya pili ni utovu wa nidhamu kwa kushindwa kutekeleza maelekezo waliyopewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa Mkoa huo, Zainab Telack,” inaeleza taarifa hiyo.

Dar es Salaam: Rais Magufuli amemsimamisha kazi kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
Amesharudi Dar?

Si alikuwa Dodoma?
 
Na manager wa TRA nae alisita kuishughulikia chadema?

Watanzania tunachanganya siasa na utendaji.
Hakuna cha siasa na utendaji hapo, wateule wote wa Rais ni makada wa chama tawala maeneo yao ya kazi,period.
 
Back
Top Bottom