Dar es Salaam: RC Makalla azuia utekelezaji wa amri ya kuzuia bodaboda na bajaji kuingia city center

You nail it!! Ulichokiongea Nathan kama wanatusikiliza na kutusoma ndio iwe ajenda yao kesho!! Mipango yoyote inatakiwa kusimamiwa na utaratibu na sheria, huwezi kuruhusu vitu kiholela ukategemea ndio kugawa riziki!! Na katika taifa lolote huwezi kuweka kila MTU akajiajiri mwenyewe
 
Hapa Makalla alichukua uamuzi kwa kukariri, akadhani kwasababu machinga imewezekana kuondolewa basi na bodaboda it will be the same, hapana haitakuwa, bodaboda na bajaji wana umuhimu zaidi kwa personal needs in case of emergency zaidi ya machinga.
 
Wakizuia boda wake kwa waume wataota vigimbi kwa kutembea kwa miguu nyakati za foleni. Ukweli ni kwamba si wote ila kuna baadhi ya madereva wa boda hawaendeshi kistaarabu wakiwa katikati ya jiji wao mda wote mi mbio tu kama vile wanawahi namba.
 
Yesu ashaondosha Korona, Bodaboda na Bajaji ndio zinaongoza kwa kuchubua magari ya wanyonge.
Bajaji wanasimama popote na ndio chanzo cha foleni,
Bajaji kutoka Ferry njia ya kati mpaka Darajani- kigamboni ile barabara imekuwa hovyo kabisa, wanaenda taratibu wakitafuta abiria huku wakikwamisha magari, waondolewe kabisa, .

Pikipiki na bajaji zimesababisha kuongezeka kwa magonjwa ya kisukari, kiriba tumbo na presha maana sasa mtu hatembei tena, kila pahala ni usafiri tu ambapo serikali inaingia hasara kubwa kuwahudumia hawa watu
 
Mwendokasi umekaa vizuri sana siku hizi, ingawa hawaendi maeneo yote. Na wenyewe wanasema hawatumii basi zote zilizopo. Tuondoe boda boda tupange mji.
 
Hapa mtoa zuia na mkaataa zuio wote wanajuana........Rc kaona huu upepo wa bodaboda na bajaj huenda ukamtoa nje ya reli,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…