Dar es Salaam to Mwanza kwa FastJet nauli ni shilingi ngapi ?

MANGUNGO

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
1,536
Reaction score
354
Wadau naomba kujua nauli ya ndege za FAST JET kutoka Dar-es-salaam hadi MWANZA ni shilingi ngapi kulingana na daraja?.... halafu unachukua mda gani kupata tarehe ya safari tangu siku mtu alipo-book au nina weza nikakata ticket leo kwa safari ya kesho na nikafanikiwa .

Maana nasikia kuna kuna ulasimu na kusubiri wadau wanaojua nipeni taarifa sahihi
 

Huo muda wa kuingia hapa kuuliza bei ya nauli ungeingia kwenye web yao ungepata majibu yote. Kama ndege ya kesho haijajaa unapata nafasi ndio, ila bei yake itakuwa kubwa ukilinganisha na aliyenunua tikiti wiki 3 zilizopita.

Hakuna madaraja na hakuna urasimu. Money talks, unaweza lipia ofisini kwao au kwa tigopesa/M-Pesa
 
Kupata bei ya kikabwela ni issue coz nilikuwa naangalia majuzi November na December nyingi zinaanzia Tsh.200,000 tax exclusive.
 
Duùh!Tanzania hovyo kabisa aisee

Kwanini unasema Tanzania ni Hovyo? Au ticket ya laki mbili kwenda mwanza umeona ni kubwa sana? Embu tupe reference ya uliko wewe kwa distanve sawa na mwanza/dar ni bei gani?
 
Kwanini unasema Tanzania ni Hovyo? Au ticket ya laki mbili kwenda mwanza umeona ni kubwa sana? Embu tupe reference ya uliko wewe kwa distanve sawa na mwanza/dar ni bei gani?

Distanve ni nini maana yake term ngumu...hemu ifafanue nielewe kwanza.
 
I mean distance! hope umenielewa ila unataka ligi isiyokuwa na maana

Teh teh teh teeeh!!sawa nimeelewa sasa,kifupi sijawahi kusafiri kwa ndege mimi wa hapa hapa ila nimepata dharula natakiwa Mwanza haraka sana.so mantiki ya mimi kusema hovyo nikutokana na tangazo lao nililowahi kusikia clouds redio kuwa Dar-Mwanza ni elfu 45...nilipoambiwa laki 2 nimestuka kwa badiriko ilo la gafla.....anyway ngoja nijipange kivingine tu dharula yenyewe sio ya pesa ntaenda tu Muro
 
Badiriko? Ilo? Gafla?
Hicho ni kiswahili?

Unauliza swali la kimasai afu unajibiwa unaleta ujuaji. Hahaha muro inakuhusu wewe
 
 
Nimekupenda, huyu anataka ligi isiyokuwa na maana, definitely that was a slip of finger on a keyboard

Sio ligi mkuu,mimi ni wa hapa hapa Tz tandale,kimsingi sijamdharau au kutaka ligi na mdau huyu,ndio maana nimemjulisha na atanielewa tu,hatupo hapa kushindana mimi mshamba sasa natafuta kueleweshwa na sio kama ilivyokurupuka na kutaka kuchochokea upuuzi...nimeuliza kwa kumaanisha.Acha hizo mtoto wa kiume wewe au mwanamke?acha dharau bhana
 
Badiriko? Ilo? Gafla?
Hicho ni kiswahili?

Unauliza swali la kimasai afu unajibiwa unaleta ujuaji. Hahaha muro inakuhusu wewe

Ujuaji hupi nilioleta?..kuna haja ya kuuliza kama nikiwa najua?..au kisa kuomba tafsiri ya distave kwa bwana kiria?..nilimaanisha na wala sikumdharau au kujifanya najua..kichwa labda kilivyo tafsiri lkn angalia muktadha wa swali kiraia na muktadha wa mimi muulizaji..hilo unalo litaka mimi siliwezi maana sikuwahi somea ualimu wa kiswahili kama na hata kama nimesoma kiswahili bado nakili sina weledi kama waunguja na pemba ambako kiswahili kiliko zaliwa na kunifikia mimi masai ...sioni jipya kwako wewe DADA
 
Hahaha. I agree with everything you said.

Na ni kweli, sina jipya.
 
Hahaha. I agree with everything you said.

Na ni kweli, sina jipya.

Haya nipe sasa mchangunuo wa safari na gharama za hao jamaa....naona umeishia kuninyea tu ..eti mimi saizi yangu Muro!aha aha aha ahaaaaaaaa!! Ni kweli kabisa sister alafu sioni noma wala kujidharau maana ni maisha pia kwasisi wa TANDALE sio nyinyi OSTA BEI aka wakishua ...alafu punguza kingereza maana mimi sijapita karibu na madarasa unaniacha bhana labda uwe unanifafanulia kidogo.
 
Walau umejicheka japo haujajidharau.

Haya, uliyosikia kuhusu urasimu ni ya uongo. Siku hizi fastjet ndo daladala za bongo. Kwa dharura nauli lazma wakubamize. Ila ukikata tiketi kama mwezi kabla unapata kwa bei rahisi. Nauli ni kati ya tzs 100,000 na 500,000 kwenda na kurudi

Ingia kwenye website yao. Angalia route unayotaka kwenda na useme kama ni kwenda na kurudi. Angalia tarehe ya kuondoka ulipo na kurudi pia. Ulikubali usisahau kuweka una mabegi mangapi manake uwanjani watakuchaji sana. Baada ya hapo unapewa bili yako.

Ukiikubali unasema utalipa baadae wanakupa reference number. Hiyo unatumia kulipia kwa mpesa ama tigo pesa. Siku ya kusafiri unataja jina tu ama kutoa kitambulisho na wataona tiketi imeshalipiwa unakwea pipa.

Siku ya kupanda ndege hakikisha umevaa viatu na socks manake hukawii kurudishwa buree. Hehehe safari njema mwaya
 
 
Wasikuchanganye bhana ..mnaangalia website gani? Mimi nimebook nakulipia Alhamic kwa ajili yakusafili alhamisi ijayo kwa 92,000. Hata ukitaka ya siku hiyohiyo unaweza kupata hata kwa 370,000. Safari za weekend bei mbaya. Ukukata wiki mbili kabla unaweza upaate kwa 60,000.
 

Aha aha aha ahaaaa!asante sana King'asti viatu na soksi ninavyo pea 2 nitavaa ndo mambo tunayotaka haya mnaojua mtutoe ushamba tusiojua japo noma kweli kidume kutolewa ushamba na mwanamama kama King'asti lkn ndio hivyo tena ulimwengu huu kukifanya unajua huku hujui ndio hayo ya kwenda mbuzi wako kwenye pipa lkn sasa nimejua kumbe viatu na soksi vinahusika basi kesho kariakoo kununua viatu na soksi mpemba mimi viatu haramu lkn ntavaa kama kafiro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…