Walau umejicheka japo haujajidharau.
Haya, uliyosikia kuhusu urasimu ni ya uongo. Siku hizi fastjet ndo daladala za bongo. Kwa dharura nauli lazma wakubamize. Ila ukikata tiketi kama mwezi kabla unapata kwa bei rahisi. Nauli ni kati ya tzs 100,000 na 500,000 kwenda na kurudi
Ingia kwenye website yao. Angalia route unayotaka kwenda na useme kama ni kwenda na kurudi. Angalia tarehe ya kuondoka ulipo na kurudi pia. Ulikubali usisahau kuweka una mabegi mangapi manake uwanjani watakuchaji sana. Baada ya hapo unapewa bili yako.
Ukiikubali unasema utalipa baadae wanakupa reference number. Hiyo unatumia kulipia kwa mpesa ama tigo pesa. Siku ya kusafiri unataja jina tu ama kutoa kitambulisho na wataona tiketi imeshalipiwa unakwea pipa.
Siku ya kupanda ndege hakikisha umevaa viatu na socks manake hukawii kurudishwa buree. Hehehe safari njema mwaya