Poa, kwa kweli sio rahisi kupata Watanzania 'asili' wenye kupanga mada jinsi ufanyavyo, yaani kupata Mtanzania ambaye hajachakachuliwa, hajasomea nje ya nchi halafu awe na uwezo huo.
Ni kweli nchi zetu hizi zinapiga hatua, na ifahamike kadiri Tanzania inapaa, ndivyo na Kenya inatoweka. Wakiamka leo waasisi wetu kutoka makaburini watashangaa na kuomba bora wazidi kuendelea kufa huko waliko.
Kenya ya leo sio ya hapo awali, tumefaulu kuthubutu, hata uwekezaji wetu nje ya nchi hususan ndani ya Tanzania umeongezeka maradufu.
Tanzania hata kama mnaendelea, lakini binafsi huwa nahisi bado mpo too slow, kila nikija Bongo na kuona fursa za uwekezaji zilizopo huwa nabaki kuwashangaa mbona mpo mpo tu na hamzichangamkii. Hiyo Mwanza unayotaja leo, nimesema mara nyingi kwamba ina uwezo wa kuwa mji mkubwa zaidi ya miji yote Afrika maana imebahatika kupachikwa katikati ya mataifa ya Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi kiasi kwamba mkiamka toka kwenye usingizi, mnaweza kufanya huo mji kuwa kitovu cha hizo nchi zote. Lakini leo hii naona mnakurupuka mara uwanja wa kimataifa Chato mara huku mara kule, hamjakaa na kuandika mikakati ya nchi.