Dar es Salaam: Wakazi Kijijini Mbezi Beach B waigomea Serikali kuhusu kuhama eneo hilo

Hilo sio eneo la makazi ni hifadhi ya barabara, waliambiwa wahame siku nyingi lakini wakawa wanakingiwa kifua na viongozi wa kata na mtaa akiwemo teja mmoja aliyekuwa anadai wasiguswe ni wapiga kura wake.

Na hata sasa hili zoezi litafail tu kwa sababu gwajima atatafutia mtaji wa kura na kwa sababu anao ushawishi mtasikia kimya na maisha yakisonga kama kawa!
 
Wakazi wa eneo la Kijijini lililopo katika Kata ya Kawe, Mtaa wa Mbezi Beach B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wamekahidi kuhama eneo hilo kama ilivyoamuliwa na Serikali.

Wakazi hao walipewa siku 14 za kuhama eneo hilo kwa hiari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Matambule.

View attachment 2819503
Mkuu wa Polisi Kawe (OCD) SP. Deus Shata, (wapili kutoka kushoto) akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Kijijini, lililoko Mbezi Beach B, kata ya Kawe, wilayani Kinondoni mwishoni mwa wiki. Wakazi wa eneo hilo walipewa siku 14 na Mkuu wa Wilaya hiyo kuondoka katika eneo hilo lakini wamekaidi. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Kawe, Husna Nondo wengine ni maofisa kutoka idara mbalimbali za Serikali.

Aidha, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kuaminika, inadaiwa kuwa, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni, Maafisa kutoka TARURA na DAWASA Novemba 17, walifika katika eneo hilo na kukuta wakazi hao wakiwa hawajatekeleza agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, ambapo, Jeshi hilo liliwataka wakazi hao hadi kufika jana saa 5 asubuhi kuwa wameshahama.

Habari za ndani zinaeleza kwamba badala ya wakazi hao kuhama kwa hiari yao, wameamua kuagiza mganga wa kienyeji kutoka mkoani Mtwara ili awafanyie zindiko wasiweze kuondoka eneo hilo.

“Kinachoendelea kwa sasa ni wananchi hao kuanza kupimana ubavu na Serikali. Badala ya kuondoka sasa wamemuagiza mganga kutoka Mtwara ili awafanyie zindiko na wanadai kuwa huyo ni Mganga wao ambaye wamekuwa wakimtumia miaka yote,” alisema mtoa habari wetu.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mtambule, aliagiza wakazi hao kuhama eneo hilo kwa hiari ndani ya 14 kama walivyoomba, lakini hadi jana maisha yalikuwa yanaendelea kama kawaida.

Mwishoni mwa wiki Polisi walifika eneo hilo ambapo pamoja na mambo mengine walishuhudia wakazi hao wakiendelea kuishi kwenye vibanda, ambavyo wamekuwa wakitumia kufanya maovu.

Uamuzi wa Serikali kutaka wananchi hao kuhama eneo hilo unatokana na mtandao wa TimesMajira Online hivi karibuni kuibua maovu yanayofanyika katika eneo hilo dogo.

Katika eneo hilo, kuna kaya kati 30-40 ambazo zinaishi katika vibanda vya mabati, ambavyo ndiyo makazi yao ya kudumu kwa takriban miaka 30.

Makazi hayo huyatumia kama sehemu zao za kufanyia biashara haramu, ambazo wao wamezihalalisha. Biashara zinazofanyika katika eneo hilo ni uuzaji wa dawa za kulevya, bangi, pombe haramu ya gongo, pombe za kienyeji na ngono ya nipe nikupe (kununua).

Biashara ya ngono ya nipe nikupe katika eneo hilo, inahusisha wanawake na wasichana wenye umri mdogo. Kinachofanyika ni maelewano na baada ya hapo, maisha yanaendelea.

Wakati wakazi wanaoishi eneo la Kijijini wakiwa wameridhika na maisha ya eneo hilo, baadhi ya wananchi waliokuwa na nyumba za kudumu jirani ya Kijijini wamezikimbia na kwenda kuishi kwingineko, kwani eneo hilo sio salama kwa malezi ya watoto na kwenye suala zima la maadili.

Mbali na hilo, pia eneo hilo limeonekana kuwa ni hatarishi kwa watoto chini ya miaka 18. Mbali na lugha chafu zinazozungumzwa na wanaofika kupata huduma, lakini kibaya zaidi watu hao wamesahau kwamba kuna vyombo vya dola.

Baada ya TimesMajira kufika eneo hilo, lilishuhudia na kujiridhisha kufanyika kwa biashara haramu na kujionea jinsi watoto wanaoishi jirani wanavyokabiliwa na tishio kubwa la kimaadili.

Chanzo: TimesMajira Online

Pia soma:
= Kijijini, Mbezi Beach eneo hatari Jijini Dar es Salaam
= Dar es Salaam: Wakazi wa Kijijini Mbezi Beach B wapewa Siku 14 Wahame
Ukitaka kumuua mbwa anza kwa kumpa jina baya.

Walianza kutungiwa makala mbaya mbaya.

Tujiulize kabla ya makala za kuwaportray kwamba ni watu waovu, je kuna matukio mangapi yameorodheshwa kufanyika hapo?

Hilo eneo lishapigwa bei kwa mwekezaji hivyo wanahamishwa ili kupisha deal la wakubwa.

Serikali kama inataka kuwahamisha, sheeia na taratibu za kuhamisha wakazi zimetumika? Au ndo Kamati ya Ulinzi na Usalama ipo juu ya sheria?

Tangu wameanza kukaa hapo na kupelekewa huduma zote, serikali ilikuwa haina habari?

Viongozi waache uhuni. Wafuate taratibu na sheria. Wagawane hizo hela na hao wakazi ama wawatafutie mahala pa kwenda.
 
watu wapo miaka 30 leo unasema waondoke kisa uhalifu kwamba huko watakapo kwenda wataacha tabia ya uhalifu

alafu kuna vyombo vyenye majukumu ya kukomesha uhalifu kwamba vimeshindwa kazi hadi chaguo iwe kuwaondoa kama ni hivyo vyombo vya usalama vifutwe sasa vina kazi gani

ama kama eneo hilo mnalitaka kijanja walipeni fidia wakajue wanafia wap sio kuwaondoa kinyemela
 
Wamakonde ndiyo walivamia hapo
Na kujenga mavibanda..
Alafu hilo eneo siyo mbali na juliana pub,sehemu hiyo imezungukwa na mashuwa ila hapo ndiyo changanyikeni

Ova
Kama ni wamakonde amini hawaami hapo. Mmakonde ukimpa kulinda nyumba yako unayojenga amini hutoaminia atakaa yeye hadi na wajukuu atapata hapo hapo. Utaishia kusema tu ile nyumba yangu ila kamwe huwezi ishi hiyo nyumba.
 
Ukitaka kumuua mbwa anza kwa kumpa jina baya.

Walianza kutungiwa makala mbaya mbaya.

Tujiulize kabla ya makala za kuwaportray kwamba ni watu waovu, je kuna matukio mangapi yameorodheshwa kufanyika hapo?

Hilo eneo lishapigwa bei kwa mwekezaji hivyo wanahamishwa ili kupisha deal la wakubwa.

Serikali kama inataka kuwahamisha, sheeia na taratibu za kuhamisha wakazi zimetumika? Au ndo Kamati ya Ulinzi na Usalama ipo juu ya sheria?

Tangu wameanza kukaa hapo na kupelekewa huduma zote, serikali ilikuwa haina habari?

Viongozi waache uhuni. Wafuate taratibu na sheria. Wagawane hizo hela na hao wakazi ama wawatafutie mahala pa kwenda.
Kuna huduma gani za kijamii wamepelekwwa hapo? Maana naona kwa upande wa umeme wanatumia solar.
 
Kama ni wamakonde amini hawaami hapo. Mmakonde ukimpa kulinda nyumba yako unayojenga amini hutoaminia atakaa yeye hadi na wajukuu atapata hapo hapo. Utaishia kusema tu ile nyumba yangu ila kamwe huwezi ishi hiyo nyumba.
Hata kwa mikocheni kwa nyerere sehemu kama hizo zilikuwepo wamakonde walikuwa wanakaa kwenye maeneo dar ambayo ni potential, hapo mbezi beach wanawatoa kwa style tu

Ova
 
Serikali huwa inakuwa wapi hawa watu wakiweka makazi yao haya maeneo ??
 
Wakazi wa eneo la Kijijini lililopo katika Kata ya Kawe, Mtaa wa Mbezi Beach B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wamekahidi kuhama eneo hilo kama ilivyoamuliwa na Serikali.

Wakazi hao walipewa siku 14 za kuhama eneo hilo kwa hiari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Matambule.

View attachment 2819503
Mkuu wa Polisi Kawe (OCD) SP. Deus Shata, (wapili kutoka kushoto) akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Kijijini, lililoko Mbezi Beach B, kata ya Kawe, wilayani Kinondoni mwishoni mwa wiki. Wakazi wa eneo hilo walipewa siku 14 na Mkuu wa Wilaya hiyo kuondoka katika eneo hilo lakini wamekaidi. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Kawe, Husna Nondo wengine ni maofisa kutoka idara mbalimbali za Serikali.

Aidha, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kuaminika, inadaiwa kuwa, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni, Maafisa kutoka TARURA na DAWASA Novemba 17, walifika katika eneo hilo na kukuta wakazi hao wakiwa hawajatekeleza agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, ambapo, Jeshi hilo liliwataka wakazi hao hadi kufika jana saa 5 asubuhi kuwa wameshahama.

Habari za ndani zinaeleza kwamba badala ya wakazi hao kuhama kwa hiari yao, wameamua kuagiza mganga wa kienyeji kutoka mkoani Mtwara ili awafanyie zindiko wasiweze kuondoka eneo hilo.

“Kinachoendelea kwa sasa ni wananchi hao kuanza kupimana ubavu na Serikali. Badala ya kuondoka sasa wamemuagiza mganga kutoka Mtwara ili awafanyie zindiko na wanadai kuwa huyo ni Mganga wao ambaye wamekuwa wakimtumia miaka yote,” alisema mtoa habari wetu.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mtambule, aliagiza wakazi hao kuhama eneo hilo kwa hiari ndani ya 14 kama walivyoomba, lakini hadi jana maisha yalikuwa yanaendelea kama kawaida.

Mwishoni mwa wiki Polisi walifika eneo hilo ambapo pamoja na mambo mengine walishuhudia wakazi hao wakiendelea kuishi kwenye vibanda, ambavyo wamekuwa wakitumia kufanya maovu.

Uamuzi wa Serikali kutaka wananchi hao kuhama eneo hilo unatokana na mtandao wa TimesMajira Online hivi karibuni kuibua maovu yanayofanyika katika eneo hilo dogo.

Katika eneo hilo, kuna kaya kati 30-40 ambazo zinaishi katika vibanda vya mabati, ambavyo ndiyo makazi yao ya kudumu kwa takriban miaka 30.

Makazi hayo huyatumia kama sehemu zao za kufanyia biashara haramu, ambazo wao wamezihalalisha. Biashara zinazofanyika katika eneo hilo ni uuzaji wa dawa za kulevya, bangi, pombe haramu ya gongo, pombe za kienyeji na ngono ya nipe nikupe (kununua).

Biashara ya ngono ya nipe nikupe katika eneo hilo, inahusisha wanawake na wasichana wenye umri mdogo. Kinachofanyika ni maelewano na baada ya hapo, maisha yanaendelea.

Wakati wakazi wanaoishi eneo la Kijijini wakiwa wameridhika na maisha ya eneo hilo, baadhi ya wananchi waliokuwa na nyumba za kudumu jirani ya Kijijini wamezikimbia na kwenda kuishi kwingineko, kwani eneo hilo sio salama kwa malezi ya watoto na kwenye suala zima la maadili.

Mbali na hilo, pia eneo hilo limeonekana kuwa ni hatarishi kwa watoto chini ya miaka 18. Mbali na lugha chafu zinazozungumzwa na wanaofika kupata huduma, lakini kibaya zaidi watu hao wamesahau kwamba kuna vyombo vya dola.

Baada ya TimesMajira kufika eneo hilo, lilishuhudia na kujiridhisha kufanyika kwa biashara haramu na kujionea jinsi watoto wanaoishi jirani wanavyokabiliwa na tishio kubwa la kimaadili.

Chanzo: TimesMajira Online

Pia soma:
= Kijijini, Mbezi Beach eneo hatari Jijini Dar es Salaam
= Dar es Salaam: Wakazi wa Kijijini Mbezi Beach B wapewa Siku 14 Wahame
Hao wapatiwe eneo jingine waondoke hapo kama watakaidi baada ya kupewa eneo hilo bakora zitembee mana kwa maelezo haya kuna ujinga mkubwa ndani ya hawa watu
 
“Kinachoendelea kwa sasa ni wananchi hao kuanza kupimana ubavu na Serikali. Badala ya kuondoka sasa wamemuagiza mganga kutoka Mtwara ili awafanyie zindiko na wanadai kuwa huyo ni Mganga wao ambaye wamekuwa wakimtumia miaka yote,”
SmartSelect_20231121_124142_Samsung Internet.jpg
alisema mtoa habari wetu.
Meakuja amekamilika
 
Hilo eneo mbona la kitambo sana
Uswaz imepitiliza
Dar hii kuna maeneo unaweza mwambia mtu kama yapo na ukashangaa,kuna eneo mbunge,mkuu wa mkoa wenyewe hawajawahi kutia
Mguu
Watu wanaishi huko na kuna utawala wao huko
Dar kuna sehemu inaitwa sogodo huko ni hatari,uhuni wote uko huko
Maisha ni ya ovyo kupitiliza

Ova
Aiseeh Sasa naanza kuelewa kwanini dada angu alini zimia sim nilipo fika dar
 
Hilo eneo mbona la kitambo sana
Uswaz imepitiliza
Dar hii kuna maeneo unaweza mwambia mtu kama yapo na ukashangaa,kuna eneo mbunge,mkuu wa mkoa wenyewe hawajawahi kutia
Mguu
Watu wanaishi huko na kuna utawala wao huko
Dar kuna sehemu inaitwa sogodo huko ni hatari,uhuni wote uko huko
Maisha ni ya ovyo kupitiliza

Ova
😂
 
Hadi sasa sijazielewa hizo sababu za kuhamishwa kuwa na mashiko...

Tuhuma zote zilizotajwa ni za jinai, na taratibi za kushughulikia tuhuma za jinai kwa mujibu wa katiba na PGO za kipoliso zinajulikana...

Watu wenye tuhuma na ushahidi usio na shaka wafikishwe kwa pilato...

Kama hayo maeneo yanapaswa kuemdelezwa, wamiliki wa sasa walipwe fidia au watafutiwe maeneo mengine wapewe makazi...
 
Back
Top Bottom