Dar es Salaam watu tupo busy pia tupo stressed sana. Kilichofanyika ni ishara ya kutujali

Dar es Salaam watu tupo busy pia tupo stressed sana. Kilichofanyika ni ishara ya kutujali

PakiJinja

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
11,689
Reaction score
25,848
Inafahamika vyema, Dar es salaam ni miongoni mwa miji yenye hekaheka sana hapa Afrika.

Kila wakati, watu tunajihisi tupo nyuma ya muda au tunadaiwa kitu, hivyo kutupelejea kila wakati tuwe mbiombio.
Dar mambo ni mengi lakini kinachofanyika hakionekani, pia faida haionekani.

Kwa kifupi tupo busy na stressed.
Dar es salaam ndiyo makao makuu ya vyombo vya habari, lakini wananchi wake hatuna habari, mambo mengi yanatupita.

Ni jambo la kujali sana pale tunapoletewa aina ya uongozi utakaotufanya tutafute muda wa kuangalia habari, itaakua ni mwanzo wa kutafuta muda wa kutulia. Aina ya viongozi watakao tutoa stress kwa kutuvunja mbavuu kwa kauli, uongeaji na matendo yao, comedy.

Ni muda wa Public therapy itakayokua ikitolewa kuanzia sasa hadi hapo utenguzi utakapotangazwa.
 
Back
Top Bottom