Dar es salaam yashika nafasi ya tano duniani

Dar es salaam yashika nafasi ya tano duniani

Kiongozi hoja yako ni ya msingi. Linalotakiwa, si kuogopa kuwapa wananchi madaraka, lakini ni kuratibu kwa utaalamu na umakini ili kuona hakuna mianya ya migawanyiko inatokea hapo mbele. Tunaweza kujifunza kwa kenya na Nigeria. Kwa vyoyote vile, lazima katiba ya nchi ndiyo isimamie masuala yote ya majimbo. Siyo kugatua in whole sale. Nigeria walifanya makosa yao wakagatua hadi central laws wakati kenya tangu ianze kuwepo imekuwa na matabaka ya ukabila ambayo hawajawahi kuyavunja.

Kwa mantiki hii uzuri na malengo mema ya decentralization yatapoteza maana ikiwa hoja itabebwa na wadandiaji wenyehila kama ccm walivyofanya kwenye katiba. Inahitaji neutral mind na utashi wa kitaifa kuratibu mfumo sahihi utakaotoa mwanya wa maendeleo na kuziba milango yote ya mipasuko ndani ya nchi.

Happy sunday.


Boko haram huku Nigeria imeletwa na sera ya majimbo au hata hili limekushinda.Kenya unaonaje ukabila.Nakwambia siku CDM ikikamata dola na kulazimisha sera ya majimbo utasikia Mtwara inataka kujitenga kwasababu ina gesi,kabla haujakaa vizuri kanda ya ziwa watasema wanataka usemi zaidi kwakuwa wanachangia zaidi na kadhalika na kadhalika.......
 
Tatizo hapa sioni nia ya kweli ya kugawa madaraka. Kinachofanyika ni maneno tu. Utasikia eti ccm wanasema wapinzania wana uroho wa madaraka, wakati wao ndio wanathibitisha uroho huo kwa kuhujumu upinzani makusudi ili waendelee kutawala hata kama hawatakiwi, na pia kwa kuzidi kucentralize maamuzi bila kujali ongezeko la population na idadi kuwa ya wataalamu nchini.

Decentralization kwa Tanzania itakuwa nguvu kwa sababu si agenda wala nia ya ccm na ndiyo sababu bado wanapma raisi madaraka ya teuzi zote na kuweka walilnzi wa matakwa yake kila mkoa na wilaya (RCs and DCs). Sana sana wakiona pressure watadandia hoja na kuifanya ovyoovyo na hata kuleta shida kubwa kwa nchi kama katiba waliyoghushi.

Lakini kwa sasa wanaikataa kwa ajili lya uroho wa madaraka, udictator na uchakachuaji wa maamuzi, na usalama wa itikadi fisadi.

Kikubwa, decentralization inatakiwa iwe planned vizuri ili kuepuka mgawanyiko na upotevu wa dhana ya utaifa.
Hii hoja imeshatajwa sana na watu. Ni nzuri na kweli naikubali sana. Watanzania hawana sababu ya kuiogopa kwa kuwa faida zake ni nyingi sana!
Devolved system of govt may just be what Tanzania needs - Letters - www.theeastafrican.co.ke
Au hata soma hapa https://www.jamiiforums.com/politic...-in-progress-but-feel-free-to-contribute.html
 
Nilidhani riport pia itasema rais wetu ni kati ya marais watano duniani ambao ni maprofessor???????????!!!!!!!!!!
 
Hatuna cha kufanya zaudi ya kuzaana labda atapatikana atakae tuondolea umasikini wetu.
 
Hatuna cha kufanya zaudi ya kuzaana labda atapatikana atakae tuondolea umasikini wetu.

Hata hawa ndugu zetu wanaofunga ndoa za mikeka asubuh na jioni kisa mohamed alifundisha na kutenda hivyo bila kuangalia nyakati nadhani watakua wanachangia sana kuuzaana sana. Huwezi kuoa wake 4 alafu ukazingatia uzazi wa mpango. Ukiwa na wake 4 utegemee kumiliki watoto wasiopungua 10. Sasa hapo unategemea nini kama sio chanza cha uchafu mijini na umasikini!!
 
Sijajua serikali imejipangaje katika mpango huu. KITABU cha Takwimu za Dunia kinachotolewa kila mwaka na Jarida la The Economist kimetoka mwaka huu na kuna baadhi ya mambo ambayo yanatakiwa kutufikirisha kama Taifa.

Kwa mfano, The Economist wametaja jiji la Dar es Salaam kama la tano duniani miongoni mwa majiji yanayokua kwa kasi duniani. Katika eneo lote la Afrika Mashariki, Dar es Salaam inazidiwa na Kampala, Uganda pekee ambayo imeshika nafasi ya tatu.

Takwimu hizo, pamoja na mambo mengine, zinaonyesha pia ya kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha kupata watoto –ambapo mwanamke mmoja anaweza kupata hadi watoto wanne. Imeshika nafasi ya 11.

Mwaka 2050, linasema jarida hilo, Tanzania itakuwa mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya watu duniani. Barani Afrika, Tanzania itakuwa ya tatu kwa idadi kubwa ya watu huku ikiwa ya 13 duniani.

Kwa sasa, jarida hilo linasema, Tanzania imeizidi Kenya kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika makazi duni (slums); ikichagizwa na ongezeko la idadi kubwa ya watu wanaohama kutoka vijijini na kuja mijini.

Swali langu ni je Serikali ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania wamejipangaje na mabadiliko haya hasa katika swala zima la miundombinu?

Wamevaa miwani ya mbao na wameweka pamba masikioni. Hutosikilizwa kamwe.
 
Back
Top Bottom