Biashara za usafiri zinahitaji usimamizi makini sana, ndiyo maana waarabu ni mamaster hapa TZ kwenye sekta hii. Hii biashara Inahitaji network sana, wewe ni jeshi la mtu mmoja, hutaki kufundisha watoto biashara na kwanza ushafeli kwenye malezi Yao toka mwanzo, una vimada kibao, nidhamu yako ilishapotea baada ya kujiona umetoboa. Sasa kama una yote hayo niliyotaja biashara ya transport hutoboi hapa TZ maana ukianguka ndo umeanguka, tena Sasa anguko lako unaliona linakuja lakini huna la kufanya maana huna pa kushika, watu wanakukataa hata unaowategemea wanakutema. Zipo kampuni za usafirishaji Tanzania toka miaka ya sabini Bado Hadi Leo zipo, ni kampuni tu ndo inabadilishwa majina.