Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha uongo Tanzania hatutumii AK47Yeah Kwa Nyagali Mdude ndichi kilitokea walipiga Juu AK47.
Mlio wake watu wote wakasambaratika
Inasikitisha sana,Mtanzania ukiacha ukondoo ni mtu mbinafsi sana."Nisaidieni naenda kuuawa, naenda kuuawa, siwajui hawa, naenda kuuawa" jamaa anapambania uhai wake nje ya Hotel ya Rovvenpec Resort iliyopo Kiluvya madukani, jijini Dar. Lakini wananchi wanashuhudia tu, na hawatoi msaada wowote. Yani ilitakiwa hicho kigari kigeuke "majivu" dakika sifuri lakini watu wanashangaa tu kama vile wanaangalia sinema.
Angalau huyu aliyechukua video amesaidia kuhabarisha umma, lakini wengine wamesimama tu wakiangalia mwenzao akilalamika kwenda kuuawa. Halafu kesho maiti yake ikiokotwa huko Ununio watu haohao wangejifanya kusikitika. Watanzania wengi ni wanafiki sana aisee. Ptuu mbaka.!
Ukifuatwa na hawa wahuni jitetee kwa nguvu zako zote, its a margin between death and life. Usitegemee watanzania maana wengi ni makondoo tu. Pigania uhai wako mwenyewe. Kama una silaha yoyote itumie kujihami. Usitembee kiboya. Huyu jamaa ubonge umemsaidia. Mungu kamjalia mwili na nguvu za kujitetea. Lakini angekua "kimbaumbau" kama mimi, saivi tungeshaandika BringBack za kutosha, au mwili wake ungeokotwa huko Ununio.
Nimejisikia vibaya sana kuona vitendo vya utekaji vinafanyika katika nchi huru na viongozi wala hawajali. Fikiria "watekaji" wanaongea kwa kujiamini kwamba "ukigoma kuingia hapo tutakuua" na bado wananchi wanashangaa tu. Pamoja na jamaa kujitetea na kufanikiwa kuokoa roho yake, bado watekaji wamejibu kwa dharau kwamba "Tutakurudia" maana yake hajakwepa kifo. Amekiahirisha tu 😭. Halafu wale tuliowapa dhamana za uongozi wanatuambia kifo ni kifo tu. Mene mene tekeli na peresi. Mungu yupo.!
Chanzo Melissa Gj .
View attachment 3150726
Watanzania wangeona ngoma ya kigodoro ungewaona wamejazana hapohatuko salama,
Nchi Ngumu hiiRaia wameshindwa hata kuchukua namba ya hiyo Gari?