DAR inatumia 50% ya Mkaa wote unaozalishwa nchini

DAR inatumia 50% ya Mkaa wote unaozalishwa nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mtalaam Mwandamizi wa Fedha kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa - Mitaji ya Maendeleo, Emmanuel Muro amesema kiasi hicho ndio chanzo kikuu cha uharibifu wa misitu kwenye mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Tanga na Lindi.

Akizungumza kupitia mdahalo ulioongozwa na Waziri wa Nishati Januari Makamba kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, amesema mikoa hiyo ambayo ni wazalishaji wakubwa wa Mkaa Tanzania pia ndiyo yenye vyanzo vingi vya maji.

Muro amesema kutokana na uharibifu unaofanyika kwenye misitu ya mikoa hiyo, imesababisha kwa kiasi kikubwa hali ya ukame na upungufu wa mvua nchini.

========================

Imeelezwa kuwa, asilimia 50 ya mkaa wote unaozalishwa nchini unatumika katika jiji la Dar es Salaam na uzalishaji huo wa mkaa ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa misitu katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Tanga na Lindi

Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba Mosi 2022 na mtalaam mwandamizi wa masuala ya fedha Shirika la Umoja wa Mataifa Mitaji ya Maendeleo, Emmanuel Muro wakati wa kongamano la nishati safi ya kupikia linalofanyika leo na kesho jijini Dar es Salaam.

Akichangia mada wakati wa mdahalo ulioongozwa na Waziri wa Nishati Januari Makamba, Muro amesema mikoa ambayo ndiyo wazalishaji wakubwa wa mkaa ndiyo chanzo cha maji yanayotiririka kwenye mito.

“Mikoa hiyo ndiyo chanzo cha maji na mito inayotiririka Dar es Salaam, ndiyo chanzo cha uhai wa jiji hili kwa hiyo ni lazima tuwe wazi sio suala la kutafuta huruma au kukipendeza. “Tusipochukua hatua sasa kukabiliana na hali hii tutafika mahali pabaya. Dar inaweza kuonekana ndogo kijiografia ila ina watu wengi na ndiyo hao watumiaji wa mkaa,” amesema Muro.

Kwa upande wake daktari Pauline Chale amesema magonjwa yanayotokana na matumizi ya nishati isiyo safi yanagharimu fedha nyingi ambazo watanzania wengi inawawia vigumu kumudu.

“Kuna mgonjwa tulikuwa tunamhudumia kwa miaka sita, alikuwa anakuja kliniki kila mwezi anachukua dawa ya Sh100,000 mwezi ulipota alishindwa kabisa kupumua ikabidi tumlaze pale hospitali kitengo cha ICU ambayo gharama yake kwa siku Sh500,000 alikaa pale kwa siku 12.

“Huyu mama hali yake ilizidi kuwa mbaya mapafu yake yakashindwa kabisa kufanya kazi akafariki dunia, hii yote ni matokeo ya matumizi ya nishati isiyo safi katika kupikia,”amesema Dk Paulina.
 
Halafu maji yanaisha Ruvu mnaanza kulalamika ooh sijui kudra za nani, kama mnaacha kuhamasisha matumizi ya gesi na nishati nyingine mbadala mnategemea kitu gani? wenzetu walioendelea walishaachana na hizo mbanga siku nyingi sana , wonders hazitakaa ziishe Afrika sio bongo tu.
 
Ivyo ndiyo wanasihasa wametufikisha. Rakini yatakwisha tu. Mungu hakipenda tutakuwa kama uraya. Hasante
 

Attachments

  • inbound7125973334093136799.jpg
    inbound7125973334093136799.jpg
    119 KB · Views: 7
Kwa jiji la Dar na swahiba wake morogoro ni aibu watu kutumia mkaa na kuni so primitive.wanaita miji ya wajanja.
 
wangeanza kugawa Bure mitingi ya gesi Dar es salaam?
wanaizungumzia tatizo badala ya kutafuta suluhu, tpdc badala ya kusambaza gesi kwa Bei nafuu wamejisambazia Kwenye majumba Yao.
 
Back
Top Bottom