KERO Dar: Jiji lenye vyanzo vingi vya maji ikiwemo Bahari lakini kila kukicha Wananchi “wana kiu ya maji”

KERO Dar: Jiji lenye vyanzo vingi vya maji ikiwemo Bahari lakini kila kukicha Wananchi “wana kiu ya maji”

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

raiamwematz24

Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
8
Reaction score
21
Dar es Salaam ni jiji lililo na mito inayotiririsha maji kuelekea baharini, lakini kwa muda mrefu kumekuwa na uhaba wa maji. Kwa muda mrefu jiji hilo limekuwa likitegemea maji ya mto Ruvu unaopita mkoani Pwani.

Wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba akiwa mto Ruvu alidai tatizo la maji ni tatizo la kidunia na Serikali itapambana sana kuhakikisha maji yanapatikana.

Naye Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alikiri kuwa ukosefu wa maji unasababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi. Lakini swali kubwa ni je, maji ndio tatizo au ufanisi wa uongozi na usimamizi wa sekta ya maji ndio hauko sawa?

Kwa muda mrefu sasa Bonde la Mto Ruvu limekuwa chanzo kikuu cha maji kwa Dar es Salaam, lakini ni wazi kabisa bado uwekezaji wake hauko sawa na ongezeko kubwa la watu na shughuli za kiuchumi katika mkoa wa Dar es Salaam.

20260121_185950.jpg
20260126_174559.jpg
Mfano wa hivi karibuni ni kisima kilichozinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Ubungo, DC Msando na mara baada ya uzinduzi, wananchi walibaini kuwa kisima hakikutoa maji kama ilivyokuwa ahadi. Hii imechochea mashaka zaidi juu ya ubora wa miradi hiyo na maswali makubwa yakiwa ni kuhusu tathmini ya kitaalamu, ufuatiliaji na uwajibikaji wa miradi husika inayohudumia wananchi.

Wakazi wa Mabibo, Manzese, Ubungo Terminal, Makoka, Kimara na Saranga wanasema mara kwa mara wanakosa maji au wanalazimika kununua maji kwa gharama kubwa kutoka kwa wafanyabiashara binafsi.

Wakati wananchi wakitaabika kwa kukosa maji, Serikali imeonekana kuelekeza rasilimali katika matumizi ya mengine kama michezo jambo ambalo ni muhimu lakini halifikii umuhimu wa maji kwani yana maslahi ya karibu na maisha ya watu.

Wakazi wa Mbezi, Kimara, Tabata na maeneo mengine ya mkoa wa Dar wanailalamikia Mamlaka ya Maji kwa kuendelea kuleta bili za maji zile zile ambazo zilikuwepo ilihali hakuna maji.

“Hii sio sawa yani bili za maji bado mnatuletea kama kawaida na maji hayatoki, tunashangaa hizi bili ni za nini na hatuoni maji?” amesema mkazi mmoja wa Mbezi.

Nao mama lishe wa Soko kuu la Mabibo wao walipeleka kilio chao kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuwa kila mara anapotoa matamko kuwa maji yatarejea mioyo yao hufurahi na kuanza kuamini kuwa serikali ina mapenzi ya dhati ya kuwasaidia lakini baadae haiwi hivyo na wanadhani wasaidizi wake huwa hawazingatii.

“Tunaiomba serikali itume wachunguzi ili wafuatilie kama maji yanatoka kweli baada ya ahadi wanazotupa viongozi wa juu kuwa tusiwe na hofu maji yatarejea ?” alisema mmoja wa wanawake hao.

Baada ya kutembelea miradi ya maji, matangi ya maji (Kimara) na visima vilivyoko Goba jijini Dar es Salaam na kuzungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo nikagundua kwamba miradi hiyo huzinduliwa ikiwa bado haijakimilika kwa asilimia zote kuja kukidhi ukosefu wa maji uliopo kwa wananchi bali hudaiwa kukamilika ili tu kuwafurahisha viongozi wa juu na wengine kunufaika kwa pesa za miradi hiyo na kutosa suala zima la ubora na uimara wake.

Nilipofika kuchunguza katika wilaya ya Ubungo wananchi walisema kwa sasa wanapitia changamoto kubwa ya maji, hali inayowafanya kuchota maji ya kisima kwa mtu ambayo bado si salama ili kupata angalau maji ya kufulia na kuoshea vyombo.

Wananchi hao wamesema hali hii imedumu kwa muda sasa hali ambayo imewafanya watembee muda mrefu wakitafta maji bila mafanikio.

20260126_174543.jpg
IMG-20260121-WA0094.jpg
IMG-20260121-WA0096.jpg

Baada ya kupokea malalamiko hayo nikajaribu kutafuta Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), ambapo watendaji wengi walijibu wapo saiti kwenye vyanzo vya maji wakifuatilia kwa ukaribu ili kuweza kurejesha huduma za maji na hawataki propaganda za wanahabari.

Kutokana na changamoto hizo, DAWASA wanapaswa kuhakikisha miradi iliyozunduliwa inafanya kazi na kuwanufaisha wananchi.

Aidha Waziri mwenye dhamana ya kuhakikisha maji yapatikana nchi nzima anao wajibu kamili wa kufanya hivyo, hakikisha maji yapatikana nchi nzima hususan mji wa Dar es Salaam ambapo ndio kitovu cha biashara na ifike wakati nchi nzima changamoto ya maji iwe ni historia.
 
Hakuna mji mkubwa duniani level ya Dar usiwe na bwawa la kutunzia maji.
 
Wakazi wa Mbezi, Kimara, Tabata na maeneo mengine ya mkoa wa Dar wanailalamikia Mamlaka ya Maji kwa kuendelea kuleta bili za maji zile zile ambazo zilikuwepo ilihali hakuna maji.
Tanzania ni FAILED STATE.

Watawala hawana akili na kutumia resources tulizonazo vizuri, wamebakia ombaomba, 10%, wanauza nje ili wanufaike wao na familia zao.

Wananchi tunaotakiwa kusimamia haya na kuhakikisha yanatekelezeka tumebakia WALALAMIKAJI (maneno tupu).

Mtu isipomfaa akili yake, utamdhuru ujinga wake.
 
Viongozi wanaotegemewa kuleta maji ya bomba ni kina madelu. Kila siku anaiongelea Chadema.
He can not address real issues. Petty men discuss petty issues.
 
Hivi hakuna permanent solution(Ufumbuzi wa kudumu) kuhusu changamoto ya maji? Nimepigiwa simu na shamba boy nimtumie hela ya kuagiza maji kwa maana ya dawasco yana week sasa hayajatoka.
 
Back
Top Bottom