Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kesi namba Cc 32444/24 inayomkabili Saleh Ayoub (39) Mkazi wa Salasala, Dar es Salaam ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres iliyopo Mbezi Africana, anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake imeshindwa kuendelea ikidaiwa shahidi upande wa Jamhuri ambaye alitakiwa kutoa ushahidi hakufika Mahakamani.
Kesi hiyo ambayo imeitwa Februari 6, 2025 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa Ushahidi, imeahirishwa mpaka Februari 17, 2025.
Hata hivyo shahidi ambaye alitarajiwa kutoa ushahidi wake (jina linahifadhiwa) amekiambia chanzo cha taarifa hii kwamba licha ya kudaiwa kutakuwepo Mahakamani, anadai kwamba alifika Mahakamani hapo tangu majira ya Saa 3:00 Asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ambayo anadai amekuwa akiifuatilia.
Anadai mpaka siku ya kesi kutajwa tangu mara ya mwisho ilipoahirishwa Januari 16, 2025 hakuwa ameupokea wito wowote wala maelezo kutoka kwa Afisa yoyote wa Mahakama yaliyolenga kumtaarifu kuwa atatakiwa kutoa ushahidi siku Februari 6, 2025.
Katika kesi hiyo Jamhuri ilieleza mbele Mh. Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa anayesikiliza Kesi hiyo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwamba watakuwa na mashahidi sita kwenye kesi hiyo.
Itakumbukwa, mshtakiwa huyo alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza siku moja baada ya Mwanachama wa Jamiiforums.com kuhoji sababu za kutofikishwa Mahakamani kwa watuhumiwa aliodai wanahusika na tukio la ukatili katika Shule ya Green Acres iliyopo Mbezi Africana.
Pia soma:
~ Ushahidi wa Kesi ya Mwalimu wa Green Acres, Saleh Ayoub anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake kuanza kutolewa Februari 6, 2025
~ Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres anayetuhumiwa kulawiti Mwanafunzi yaahirishwa Mwezi mzima, Hakimu apata udhuru
~ Watu 6 kutoa ushahidi Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake
~ Dar: Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi wake afikishwa Mahakamani
~ Walimu wa Shule ya Green Acres (Dar) wanaotuhumiwa kulawiti na kuwadhalilisha Wanafunzi, wanalindwa na nani?