Lissu Mungu akusimamie sana, Utashinda kwa nguvu ya Mungu
Lissu sijui yupo na dam gani, hakuna kipindi alikua na vizingiti ,wakati agombea urais wa TLS , ila alipita ,pamoja kwamba alifika ukumbini amechelewa akitokea Dar, kutokana na kesi kama sikumbuki, ila inasemekana baada ya kufika ukumbini , Alitema hotuba ya hatari , ambayo ilimshangaza kila wakili Msomi.
2020 wakati wa kugombea urais wa nchi ,alikutana na vikwazo vingi kutoka tume, mnakumbu mpaka anakamilisha taratibu ilikua usiku ,ila alipenya na kupeperusha bendera ya chama, kama uchaguzi ule ungekua huru ,leo tungekua tunaongea mengine.
Ila mwamba alilambishwa risasi 16, akuushinda umauti na yupo njema kuliko jana.
Sasa hii ya chadema wala sina shaka ,mapema sana biashara inaisha.
MBOWE amekua akishinda tokana na aina ya wagombea aliokua anakutana nao, lakini pia aina za nyakati za vipindi vile.
Lissu ndo mwenyekiti ajae