Dar: Kijana auawa kwa kuchomwa moto kwa tuhuma za kuiba laki mbili

Shing Yui

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
15,168
Reaction score
38,049
Jumanne Juma(26), mkazi wa Mtaa wa Kimara B, wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, ameuawa na watu aliokuwa akiwafanyia kazi za nyumbani kwa kumchoma na Petrol usiku wa Januari 23, 2025 wakidai amewaibia kiasi cha shilingi laki mbili kwenye mkoba alipoenda kudai malipo yake.

Akiongea na EATV, mke wa marehemu Helen Mariki anasema watu waliomuua mme wake walimfata nyumbani saa4 usiku wakimtaka wakamlipe hela anayowadai pamoja na kumpa kazi nyingine ndipo wakaagiza mafuta ya Petrol kwa ajili ya kumchoma kwa sababu amewaibia.

Mwenyekiti Mtaa wa Kimara B Beruk Kikwala, amethibitisha tukio hilo kutokea ambapo baada ya kupata taarifa aliwaagiza Polisi Jamii kwenda kuwadhibiti waliotekeleza tukio hilo mpaka Jeshi la Polisi lilivyofika na kuwatia nguvuni.


Your browser is not able to display this video.
 

Umasikini buana, yaani kupoteza laki mbili tu ndio uchome mtu moto
 
Watuhumiwa wameshakamatwa na wapo ndani mahabusu au bado?
Ni vyema wakakamatwa huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…