Dar: Kuna mgomo wa wafanyabiashara Manzese?

Mshobaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
1,714
Reaction score
677
Wakuu nimefika eneo la maduka ya Manzese kwa ajili ya kufanya manunuzi yangu binafsi ila nikakuta maduka yote yamefungwa.

Kwa tetesi zilizopo ni kwamba kuna mgomo unaoendelea.

Tatizo kubwa ni halmashauri kuweka service levy kubwa ambazo hazina uhalisia walikuja viongozi wakasema majibu kamili watayatoa hapo kesho saa mbili na ndipo wafanyabiashara wakasema wanasubiri majibu ndipo watafungua maduka.

=====

UPDATES 22 Mei 2024

=====

Shughuli za biashara katika baadhi ya maduka kwenye eneo la Manzese jijini Dar es Salaam yalisimama kwa muda leo Mei 22, 2024 baada ya wafanyabiashara kufunga maduka wakitaja sababu kuwa ni ushuru.

Hata hivyo wafanyabiashara hao walifungua maduka hayo baada ya Katibu Tawala wa Dar es Salaam, Tobą Nguvila kukutana nao na kufanya kikao cha zaidi ya saa tano huku akieleza kuwa chanzo cha mgomo huo kilikuwa uelewa mdogo wa wafanyabiashara hao kuhusu elimu ya kodi.

Je, wafanyabiashara wa maeneo yenu wana elimu ya kutosha kuhusu malipo ya kodi kwa TRA?

Chanzo: Azam TV
 
Leo inaenda Siku ya tatu huduma hazipatikani tunaomba suluhisho ya hili tatizo wahusika
 
Wakuu nimefika eneo la maduka ya Manzese kwa ajili ya kufanya manunuzi yangu binafsi ila nikakuta maduka yote yamefungwa.

Kwa tetesi zilizopo ni kwamba kuna mgomo unaoendelea.

Tatizo kubwa ni halmashauri kuweka service levy kubwa ambazo hazina uhalisia walikuja viongozi wakasema majibu kamili watayatoa hapo kesho saa mbili na ndipo wafanyabiashara wakasema wanasubiri majibu ndipo watafungua maduka.
Maduka ya bidh bidhaa gani mkuu
 
INGEKUWA KARIAKOOOO MAWAZIRI WAKUU WA. .. HAOOO

KWAKUWA MANZESE PAMBANEN NA HALIZENU

NCHITAMUUSANAHII
 
Wakuu nimefika eneo la maduka ya Manzese kwa ajili ya kufanya manunuzi yangu binafsi ila nikakuta maduka yote yamefungwa.

Kwa tetesi zilizopo ni kwamba kuna mgomo unaoendelea.

Tatizo kubwa ni halmashauri kuweka service levy kubwa ambazo hazina uhalisia walikuja viongozi wakasema majibu kamili watayatoa hapo kesho saa mbili na ndipo wafanyabiashara wakasema wanasubiri majibu ndipo watafungua maduka.
Service Levy bei imewekwa kiasi gani mkuu?.

Mnafanya malipo kwa control number au cash?
 
Back
Top Bottom