Dar kwenda Mbeya na passo

Dar kwenda Mbeya na passo

Mazee habari,nauliza kama naweza kwenda Mbeya toka Dar na ka gari kangu haka kadogo ka toyota Passo nina dharula kidogo,na kwa wazoefu mafuta ya kiasi gani naweza tumia,ka passo kenyewe ni kale kadogo ka pistoni 3....kwa mzoefu naomba anidaidie!
Piston tatu noma azima gari ingine..
 
Wanaume tutafute hela asee. Makonda anatunyanyasa sana
 
Nimekupenda bure mkuu, nipo karibu kununua kigari changu cha kuendea job. Nitakutafuta unipe elimu hata kwa gharama.
Usijali mkuu, bila gharama yoyote. Mambo mengine ni kusaidiana ushauri tu
 
je, unapotoka safari ndefu na gari za cc chini ya elfu mbili unatakiwa kuiacha silence kwa muda gani kabla ya kuizima?
Gari yoyote (ikiwa haina turbo) haijaalishi CC, ukifika destination yako izime tu. hapo ndio engine itapowa. Kwa gari ambayo ni nzima, ukitizama geji ya temperature utaona imekaa kati kati constant ukiwa safarini. hio maana yake gari iko cooled sawa sawa inavotakiwa. kwaio ukisimama ukaweka silence, mshale utabaki pale pale kati, kwaio hakutakuwa na tofauti yoyote ukiizima apo apo au ukiiacha kwa mda kidogo. ila ukitaka engine ipoe, izime apo apo haina haja ya kusubiri kwa sababu ukisubiri haipowi inaendelea kupata moto, tena kwa vile umepiga safari ndefu utakuta feni zinapepea mda mrefu sana kwa sababu engine haipoi ila inazidi kupata moto ikikaa silence.

Ni gari yenye turbo ndio unashauriwa kusubiri kwanza, kwa sababu turbo inakuwa cooled na oil.
 
Ila akiona mwenye paso kama yake lazma ampeleke mbio ili zikifa zife zote asikubali kupata hasara peke yake[emoji23][emoji23][emoji23]
Haswa kwa gari ndogo aliyonayo asikimbizane na Crown, Altezza, Subaru wala Land Cruiser yeye awe mpole tu afike salama
 
Ist ni gari kubwa sana cc1200 na kuendelea af piston 4 paso ni 3 na ni cc ndogo
 
Mkuu,
Kwa uzoefu wangu wa Passo Dsm - Mby hadi Ichenjezya kwetu inatoboa kabisa. Shida kidogo ni kupanda mlima Kitonga gari ilikuwa inasinzia sana, so inahitaji kuibembeleza, pale usiwe na haraka panda taratiibuu hadi kwa wachoma mahindi pale juu then fungua.

Mkuu, Kwa ujumla kama walivyo shairi GT wengine before, jiepushe kufanya ligi Vs drivers wenyeharaka zao na magari ya nguvu. Be yourself but determined.

Kuhusu wese, hiyo ndiyo raha ya kipekee kwa gari hiyo. Ukianza na full tank na ili uwe amani na fuel gauge, Unaweza kujazilizia Mkm, Mafinga or Makambako, then upo Mafiat.

SAFARI NJEMA MKUU.!!
Ukiona gari inachoka mlimani inapashwa iangaliwe vyema ,kama ni automatic kuna shida kidogo hasa kuna kichujio hapo ndani ya gear box inapashwa kusafishwa, au mfumo wa mafuta hasa izi gari za kisasa usipo kuwa sawa nawenyewe ni tatizo pia.
 
Gari yoyote (ikiwa haina turbo) haijaalishi CC, ukifika destination yako izime tu. hapo ndio engine itapowa. Kwa gari ambayo ni nzima, ukitizama geji ya temperature utaona imekaa kati kati constant ukiwa safarini. hio maana yake gari iko cooled sawa sawa inavotakiwa. kwaio ukisimama ukaweka silence, mshale utabaki pale pale kati, kwaio hakutakuwa na tofauti yoyote ukiizima apo apo au ukiiacha kwa mda kidogo. ila ukitaka engine ipoe, izime apo apo haina haja ya kusubiri kwa sababu ukisubiri haipowi inaendelea kupata moto, tena kwa vile umepiga safari ndefu utakuta feni zinapepea mda mrefu sana kwa sababu engine haipoi ila inazidi kupata moto ikikaa silence.

Ni gari yenye turbo ndio unashauriwa kusubiri kwanza, kwa sababu turbo inakuwa cooled na oil.
Ahsante sana mkuu madereva wengi tumeaminishwa kutokuzima gari baada ya safari ndefu na badala yake ibaki on kwa muda kidogo. Ahsante mkuu.
 
Ahsante sana mkuu madereva wengi tumeaminishwa kutokuzima gari baada ya safari ndefu na badala yake ibaki on kwa muda kidogo. Ahsante mkuu.
Wanasababisha watu kupoteza mafuta bure bure tu....

Ukitaka kujua kama gari ikikaa silence haipoi, chomoa switch za feni halafu wacha radiator ifanye kazi bila ya hizo feni, utaona temperature inavopanda na kuzidi kati kati ya inapotakiwa bila kusimama. Yaani hii experiment ifanye hata kama ndo kwanza unaamka asubuhi na kuwasha gari lako, utajionea engine inavopata moto na kukaribia kuzima yenyewe.
 
Uko vizuri mkuu
 
Watajuaje ana gari?
Kwenda safari na chombo binafsi haina maana kuwa unataka kuonyesha watu una gari....napingana na wewe

Kama mtu mfuko wake unaruhusu kuna uzuri wa kusafiri na private car...

....utaendesha mwendo uutakao wewe

....utasimama kula au kupumzika sehemu uitakayo wewe..

....huko uendako utapunguza purukushani za kukodi boda boda, bajaji, taxi au kuazima magari ya ndugu au marafiki ili kufanikisha shughuli iliyokupeleka

....unaweza kuanza safari kwa muda unaotaka wewe.

Mwisho, maisha ya sasa si ya zamani....gari si kitu cha maonyesho..ni one of basic needs kama uchumi wako unaruhusu.
 
Ndio akili yako ilipoishia,...ndio nyinyi mpaka leo mnaona kuwa na gari ni ufahari....wakati nowadays gari ni basic need,na unaamua kuwa na gari ili ikurahisishie maisha,....ubovu watanzania tunaona sifa kuwa masikini.....,sasa ka gari kama haka ka passo ambako mtu yeyote akijipanga ananunua wewe kichwani mwako unawaza ufahari.,....tujifunze kuficha upumbavu wetu kwa kukaa kimya....!
Bora umempa za uso huyo mkolomijè
 
Back
Top Bottom