Dar: Machinga waongezewa siku 12 kuhama kwenye maeneo yasiyo rasmi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imewaongezea siku 12 wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) kuanzia leo wahame katika maeneo yasiyo rasmi wanayofanyia biashara zao.

Awali Serikali ya mkoa huo iliagiza kuwa leo ndiyo iwe mwisho kwa wafanyabiashara hao kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi. Uamuzi wa kuongeza siku hizo 12, umetolewa leo, Jumatatu Oktoba 18,2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo kuhusiana na mpango wa kuwaondoa.

Makalla amesema ameamua kuwapa muda huo ili kila mmoja aweze kwenda katika eneo atakalokuwa amepangiwa na baada ya hapo hatataka kusikia kisingizio chochote.

"Nawapa muda mpaka Oktoba 30, baada ya hapo sitaki kusikia kisingizio chochote labda mtu aje na malalamiko kwamba kaenda kwenye maeneo yaliyotengwa kakosa nafasi," amesema Makalla. Makalla ametaja maeneo ambayo wafanyabiashara hao wanatakiwa kuondoka kuwa ni kwa wale walio juu ya mifereji na mitaro, kwenye hifadhi za barabara na mbele ya shule za Serikali au taasisi za Serikali.

Maeneo mengine wasiotakiwa kuwepo wafanyabiashara hao ni njia za waenda kwa miguu na wale waliopo mbele ya biashara za maduka ya watu.

Mwananchi
 
Nimepita pale CBE Pamekuwa pasafi, sijajua IFM na wizara ya afya hali yake ilivo,
 
Ni jambo jema kuliko watu kupigwa au kuvunjiwa vitu vyao,jambo likifanyika kwa hiari na kwa amani huleta umoja na mshikamano.
 
Hakuna kujipanga wanatakiwa wapangwe
Sijajua vizuri pale kama wamepangwa au wamejipanga lakini nilivyoona haki ya kila mtumiaji imezingatiwa na mimi binafsi hiyo ndio ilikuwa kero yangu kubwa kwamba machinga waliamua kujimilikisha kila eneo kuanzia barabara za gari,njia za waenda kwa miguu n.k
 
HUKU KWETU TEGETA KUMEPENDEZA SANA. UKISIMAMA TEGETA KWA NDEVU, TEGETA KIBAONI UNAIONA WAZI WAZI. CHANGAMOTO MPYA NI UCHAFU ULIYOJAA KWNY MITARO. NA NILIPITA MAENEO YA KARIAKOO, KUHUSU WAMACHINGA WALIYOPO MBELE YA MADUKA, MHHH! NAPATA UKAKASI SIJUI KAMA WATAONDOKA? LAKINI NADHANI ZOEZI LINAENDELEA VIZURI. YAANI WANANCHI WANANCHI WANATII SHERIA BILA SHURUTI
 
Tumejipanga vema sana kumaliza hili jambo
 
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imewaongezea siku 12 wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) kuanzia leo wahame katika maeneo yasiyo rasmi wanayofanyia biashara zao.

Awali Serikali ya mkoa huo iliagiza kuwa leo ndiyo iwe mwisho kwa wafanyabiashara hao kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi. Uamuzi wa kuongeza siku hizo 12, umetolewa leo, Jumatatu Oktoba 18,2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo kuhusiana na mpango wa kuwaondoa.

Makalla amesema ameamua kuwapa muda huo ili kila mmoja aweze kwenda katika eneo atakalokuwa amepangiwa na baada ya hapo hatataka kusikia kisingizio chochote.

"Nawapa muda mpaka Oktoba 30, baada ya hapo sitaki kusikia kisingizio chochote labda mtu aje na malalamiko kwamba kaenda kwenye maeneo yaliyotengwa kakosa nafasi," amesema Makalla. Makalla ametaja maeneo ambayo wafanyabiashara hao wanatakiwa kuondoka kuwa ni kwa wale walio juu ya mifereji na mitaro, kwenye hifadhi za barabara na mbele ya shule za Serikali au taasisi za Serikali.

Maeneo mengine wasiotakiwa kuwepo wafanyabiashara hao ni njia za waenda kwa miguu na wale waliopo mbele ya biashara za maduka ya watu.

Mwananchi
Kumbe tulio mbele ya makanisa na misikiti hatuhusiki, asante baba.
 
Jamaa kakomaa Sana na kafanikiwa niliona msukuma alitaka support ya wadai alipoona hakuna amenywea kbs

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna kujipanga wanatakiwa wapangwe
Hapa ndio wanasababisha usumbufu mkubwa hadi mfugale bridge haiwezi kufanya kazi iliyokusudiwa!! Cha kuzingatia wasije kuwafanya waliohama kuanza kurudi tena kwa muda huo wa siku 12
 
Back
Top Bottom