Dar: Machinga waongezewa siku 12 kuhama kwenye maeneo yasiyo rasmi

Dar: Machinga waongezewa siku 12 kuhama kwenye maeneo yasiyo rasmi

Pia hamtakiwi kwani mnaweza kupata hitilafu na moto kuanza na kusababisha madhara kwa mkusanyiko mkubwa
Hatuuzi gesi, tunauza soda, juisi na maji vyote havilipuki, pia pipi na aisikirimu, pia hailipuki.
 
Wameongeza na wamachinga waliohama wameanza kurudi tena, wametelekeza maeneo waliyopewa.
 
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imewaongezea siku 12 wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) kuanzia leo wahame katika maeneo yasiyo rasmi wanayofanyia biashara zao.

Awali Serikali ya mkoa huo iliagiza kuwa leo ndiyo iwe mwisho kwa wafanyabiashara hao kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi. Uamuzi wa kuongeza siku hizo 12, umetolewa leo, Jumatatu Oktoba 18,2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo kuhusiana na mpango wa kuwaondoa.

Makalla amesema ameamua kuwapa muda huo ili kila mmoja aweze kwenda katika eneo atakalokuwa amepangiwa na baada ya hapo hatataka kusikia kisingizio chochote.

"Nawapa muda mpaka Oktoba 30, baada ya hapo sitaki kusikia kisingizio chochote labda mtu aje na malalamiko kwamba kaenda kwenye maeneo yaliyotengwa kakosa nafasi," amesema Makalla. Makalla ametaja maeneo ambayo wafanyabiashara hao wanatakiwa kuondoka kuwa ni kwa wale walio juu ya mifereji na mitaro, kwenye hifadhi za barabara na mbele ya shule za Serikali au taasisi za Serikali.

Maeneo mengine wasiotakiwa kuwepo wafanyabiashara hao ni njia za waenda kwa miguu na wale waliopo mbele ya biashara za maduka ya watu.


Mwananchi
Makalla kanifurahisha kwenye maeneo wasiotakiwa kuwepo, hapo chinga ni marufuku kariakoo
 
Jamaa kakomaa Sana na kafanikiwa niliona msukuma alitaka support ya wadai alipoona hakuna amenywea kbs

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
Wala sio kuwa amekomaa!!bila support ya Rais , asingefanikiwa, kwani, kipindi anatoa kauli tu, walianza kuibuka watu wengi hasa wanasiasa, wakaanza kumsema kuwa hao wamachinga ni wapiga kura wao waende wapi, sasa siku ile mama alipochomekea tu kuhusu kuwa wamachinga wanatakiwa wafuate maelekezo wanayopewa kwani miji haiwezi kuwa hivi, ndio ma RC'S wote wakapata nguvu na wale wanasiasa uchwara sikuwasikia tena!!!kwani wengi walijua Makala atafukuzwa kazi kama wale wa Morogoro.
 
Hatuuzi gesi, tunauza soda, juisi na maji vyote havilipuki, pia pipi na aisikirimu, pia hailipuki.
Ule umeme na mbao na makarabrasha yanayotumika kujenga hivi vibanda in rahisi kushika moto na kusababisha maafa katika mkusanyiko, labda hizo taasisi wajenge vibanda spesho na kuvikodishia kwa utaratibu
 
Back
Top Bottom