Dar: Machinga waongezewa siku 12 kuhama kwenye maeneo yasiyo rasmi

Pia hamtakiwi kwani mnaweza kupata hitilafu na moto kuanza na kusababisha madhara kwa mkusanyiko mkubwa
Hatuuzi gesi, tunauza soda, juisi na maji vyote havilipuki, pia pipi na aisikirimu, pia hailipuki.
 
Wameongeza na wamachinga waliohama wameanza kurudi tena, wametelekeza maeneo waliyopewa.
 
Makalla kanifurahisha kwenye maeneo wasiotakiwa kuwepo, hapo chinga ni marufuku kariakoo
 
Jamaa kakomaa Sana na kafanikiwa niliona msukuma alitaka support ya wadai alipoona hakuna amenywea kbs

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
Wala sio kuwa amekomaa!!bila support ya Rais , asingefanikiwa, kwani, kipindi anatoa kauli tu, walianza kuibuka watu wengi hasa wanasiasa, wakaanza kumsema kuwa hao wamachinga ni wapiga kura wao waende wapi, sasa siku ile mama alipochomekea tu kuhusu kuwa wamachinga wanatakiwa wafuate maelekezo wanayopewa kwani miji haiwezi kuwa hivi, ndio ma RC'S wote wakapata nguvu na wale wanasiasa uchwara sikuwasikia tena!!!kwani wengi walijua Makala atafukuzwa kazi kama wale wa Morogoro.
 
Hatuuzi gesi, tunauza soda, juisi na maji vyote havilipuki, pia pipi na aisikirimu, pia hailipuki.
Ule umeme na mbao na makarabrasha yanayotumika kujenga hivi vibanda in rahisi kushika moto na kusababisha maafa katika mkusanyiko, labda hizo taasisi wajenge vibanda spesho na kuvikodishia kwa utaratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…