Dar: Mahakama yatupa mbali pingamizi katika kesi ya Mbowe

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Akisoma uamuzi huo leo Jumatatu Novemba 15, 2021 Jaji Joachim Tiganga amekubaliana na hoja za upande wa mashitaka na kukubali barua iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama itolewe kama kielezo na Shahidi namba mbili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Mawakili upande wa utetezi walipinga kuhusiana na barua ambayo upande wa mashtaka uliomba kuiwasilisha mahakamani kupitia kwa shahidi wa pili katika kesi hiyo ndogo.

Upande wa mashtaka Ijumaa iliyopita kupitia kwa shahidi huyo wa pili uliiomba mahakama iipokee barua hiyo ya msajili inayoonesha kuwa upande wa mashtaka umeomba kitabu cha kumbukumbu za Mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam cha mwaka 2020, ili shahidi huyo aweze kukiwasilisha mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wake na kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Chanzo: Mwananchi
 
AIgmal.jpg
 
Wahudumu Uchumi halisi hapa Tanzania wanatembelea magari ya kifahari, na wanaishi ktk majumba ya kifahari sana na wanazidi kuhujumu Uchumi wetu ila hawajawahi kufikishwa kortini kwa sababu serikali ipi mikononi mwao.

Leo huyu mangi retired dj anashitakiwa kwa kosa la kuhujumu Uchumi, oooh mara ni gaidi, hii ni kweli kuhusu hizo tuhuma?

Acha jua lizidi kutelemka maana haki zimeporwa
 
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Akisoma uamuzi huo leo Jumatatu Novemba 15, 2021 Jaji Joachim Tiganga amekubaliana na hoja za upande wa mashitaka na kukubali barua iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama itolewe kama kielezo na Shahidi namba mbili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Mawakili upande wa utetezi walipinga kuhusiana na barua ambayo upande wa mashtaka uliomba kuiwasilisha mahakamani kupitia kwa shahidi wa pili katika kesi hiyo ndogo.

Upande wa mashtaka Ijumaa iliyopita kupitia kwa shahidi huyo wa pili uliiomba mahakama iipokee barua hiyo ya msajili inayoonesha kuwa upande wa mashtaka umeomba kitabu cha kumbukumbu za Mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam cha mwaka 2020, ili shahidi huyo aweze kukiwasilisha mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wake na kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Chanzo: Mwananchi
MBOWE na CHADEMA waondoe mawakili mahakamani hapo ili hao wateule wa mwenyekiti wa CCM wafanye walitakalo bila pingamizi lolote.

Uwepo wa mawakili ni upotezaji wa muda. Liwalo na liwe MBOWE atafungwa kifungo cha maisha.

Hayo ndio matakwa na mapendekezo ya nzi wa kizungu
 
NASUBIRI MAONI YA ERYTHROCYTE KUHUSU ABUBAKAR MBOWE NA IGAIDI WAKE
 
Hawa mawakili wamuhurumie mwenzao,haya mapingamizi kila siku,yanachelewesha kesi kuisha,wao wakipa pesa na kujitangaza kibiashara tu.
 
Huyu baba akichomoka kwenye hii kesi natamani achane na Siasa anapigania kitu ambacho kwa sasa hakiwezekani kupatikana labla kwa kizazi kijacho
 
Hawa mawakili wamuhurumie mwenzao,haya mapingamizi kila siku,yanachelewesha kesi kuisha,wao wakipa pesa na kujitangaza kibiashara tu.
hiyo ni mipango ya kibatala na lissu siunaona lissu yuko kimya ? mbowe anafungwa hakuna wakili anayemtetea hapo wote wanamuangamiza
 
MBOWE na CHADEMA waondoe mawakili mahakamani hapo ili hao wateule wa mwenyekiti wa CCM wafanye walitakalo bila pingamizi lolote.

Uwepo wa mawakili ni upotezaji wa muda. Liwalo na liwe MBOWE atafungwa kifungo cha maisha.

Hayo ndio matakwa na mapendekezo ya nzi wa kizungu
Nadhani ni bora waendelee ili Dunia ione na sisi Wananchi tumejifunza mambo mengi kuhusu Taifa letu na Wadhalimu wanaotuongoza.
 
MBOWE na CHADEMA waondoe mawakili mahakamani hapo ili hao wateule wa mwenyekiti wa CCM wafanye walitakalo bila pingamizi lolote.

Uwepo wa mawakili ni upotezaji wa muda. Liwalo na liwe MBOWE atafungwa kifungo cha maisha.

Hayo ndio matakwa na mapendekezo ya nzi wa kizungu
Yani hili ndilo linalotakiwa kufanywa.Kama ukweli unakataliwa waziwazi ni kwamba hili wameshaliamuwa la kumfunga wasipoteze muda.
toa mawakili wote acha waamue walitakalo.Mwendazake mipango yake yote kumbe ilikuwa ni kulikimbilia kabuli.
Sasa hawa wanaojiona wataishi milele ni kuwaachia to tuone watafika wap na mipango yao miovu...
 
Back
Top Bottom