Dar: Mchungaji wa Nigeria anayedaiwa kukutwa na Heroin afariki gerezani

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mchungaji na mfanyabiashara raia wa Nigeria, Henry Ozoemena, anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha kilo 20 za dawa za kulevya aina ya Heroine, amefariki dunia baada ya kupata shambulio la moyo akiwa mahabusu katika gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam.

Wakili Yasin ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Ijumaa Desemba 30, 2022, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rhoda Ngimilanga wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Ozoemena (47) na wenzake wawili raia wa Lativia, ambao ni Linda Mazure (24) na mchumba wake Martins Plavins (23), wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 61/2021, yenye mashtaka ya kusafirisha dawa hizo za kulevya.

Mchungaji huyo alidakwa April 2019 na Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya katika nyumba iliyopo Mtaa wa Pemba, Kariakoo, Dar es Salaam.

Wakili wa Ozoemena, Hassan Yasin ametoa taarifa hiyo, Mahakama hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rhoda Ngimilanga, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Yasini ambaye alishika mikoba ya wakili Elipatra Ali, amedai mahakamani hapo mteja wao aliugua akiwa gereza la Segerea baada ya kupata madhara ya shambulio la moyo.

Amedai Ozoemena aliaguka wakati anatembea katika gereza hilo na alipopelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ndio ilibainika kuwa alipata shambulio la moyo na wakati akipatiwa matibabu alifariki dunia.

Wakili huyo amedai mteja wao walifariki wiki mbili zilizopita na tayari mwili wake umesafirishwa kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya mazishi.

Awali, Wakili wa Serikali Faraja Ngukah aliieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Ngukah baada ya kueleza hayo, wakili Yasini aliomba upande wa mashtaka kukamilisha haraka taratibu za kusajili taarifa na nyaraka muhimu Mahakama Kuu ili kesi hiyo iweze kuendelea.

"Mheshiwa hakimu, kesi hii ni ya muda mrefu na washtakiwa wapo ndani hawana dhamana, hivyo ni vyema upande wa mashtaka wakafanya haraka kusajili taarifa muhimu Mahakama Kuu ili kesi hii iweze kuendelea kwa hatua nyingine" amedai wakili Yasini

Pia, wakili Yasin ameiomba siku kesi hiyo itakapoitwa mahakamani hapo, washtakiwa wapelekwe mahakamani ili waende kuonana na kiongozi wa Waendesha Mashtaka Mahakama ya Kisutu.

Akijibu hoja hizo, wakili Ngukah amedai atahakikisha nyaraka hizo zinasajiliwa mapema iwezekanavyo ili kesi hiyo hiyo iweze kuendelea.

Kuhusu hoja ya washtakiwa kueletwa mahakamani, wakili Ngukah amedai" Tutakapokamilisha kusajli nyaraka hizo, washtakiwa wataletwa mahakamani na kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo, hivyo sioni ulazima wa kuwaleta washtakiwa mahakamani hapa kwa kuwa wakili wao yupo hapa."

Hata hivyo, kesi hiyo imeendeshwa kwa njia ya video conference huku washtakiwa wakiwa mahabusu.

Hakimu Ngimilanga baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha mapema kusajili nyaraka hizo ili kesi iweze kuendelea kwa kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ngimilanga ameirisha kesi hiyo hadi Januari 13, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wapo gerezani kutokana na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Itakumbukwa kuwa April 7, 2021 washtakiwa hao walisomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo (Commital Proceedings) baada ya upelelezi wake kukamilisha, lakini baadae kesi hiyo ilifutwa na kufunguliwa nyingine yenye mashtaka kama hayo.

Katika mashtaka yao, Linda anadaiwa Aprili 17, 2019, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam( JNIA), alikutwa akisafirisha dawa za kulevya ndani ya mabegi mawili yenye rangi ya brouni na nyeusi, moja lina kilo 15.8 na lingine kilo 4.8 za Heroine.

April 19, 2019 alikamatwa Plavins eneo la Kariakoo Dar es Salaam na alikiri kumsafirisha Linda kutoka Lativia kuja Tanzania kuchukua dawa hizo za kulevya na walikuwa wakiishi wote King's Hotel.

Muda mfupi baadae, alikamatwa, Ozoemena na katika mahojiano na jeshi la polisi alikiri kumpatia Linda bengi moja lilikuwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 15.8, wakati walipokutana na Plavins hotelini.

Mbali shtaka la kusafirisha dawa za kulevya, Ozoemena anakabiliwa na shtaka la kuishi nchini bila kuwa na kibali kwani aliingia nchini Julai mosi, 2017 na wakati anakamatwa kibali chake cha matembezi kilikuwa kimeisha muda mrefu.

MWANANCHI
 
Wachungaji wengi huwa wana bambikiziwa hizi kesi za madawa,
Hata T.B Joshua alishabambikiziwa na anti-christ waliopo kwenye serikali
 
Uongo mtupu huyo mchungaji atakuwa CCM na DDP kachukua pesa na kumuachia tu, maana DDP wasasa yupo pale kuwaachia huru wahujumu uchumi tena wageni
 
Wachungaji wengi huwa wana bambikiziwa hizi kesi za madawa,
Hata T.B Joshua alishabambikiziwa na anti-christ waliopo kwenye serikali
Tena huko Nigeria upinzani mkubwa wa Ukristo na Uislam , Muislam hataki kuona Mkristo akifanya miujiza , so anamchafua
huna akili.
 
Pamoja na kwamba tunaimani moja kulingana na hii comment,ila sidhani kama upo sahihi
 
Awamu hii mbona hatusikii wauza madawa ya kulevya wakikamatwa na kushtakiwa kama awamu ile iliyopita? Au kile kitengo chetu cha kupambana na madawa ya kulevya kipo likizo? Au kinasubiri kiongozi mungine aina ya JPM aje ndo waanze tena kazi ya kamata kamata?
 
Da es Salaam. Mchungaji na mfanyabiashara raia wa Nigeria, Henry Ozoemena, anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha kilo 20 za dawa za kulevya aina ya Heroin, amefariki dunia baada ya kupata shambulio la moyo akiwa mahabusu katika gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam.

Wakili Yasin ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Ijumaa Desemba 30, 2022, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rhoda Ngimilanga wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Ozoemena (47) na wenzake wawili raia wa Lativia, ambao ni Linda Mazure (24) na mchumba wake Martins Plavins (23), wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 61/2021, yenye mashtaka ya kusafirisha dawa hizo za kulevya.

Mchungaji huyo alidakwa April 2019 na Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya katika nyumba iliyopo Mtaa wa Pemba, Kariakoo, Dar es Salaam.

Wakili wa Ozoemena, Hassan Yasin ametoa taarifa hiyo, Mahakama hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rhoda Ngimilanga, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Yasini ambaye alishika mikoba ya wakili Elipatra Ali, amedai mahakamani hapo mteja wao aliugua akiwa gereza la Segerea baada ya kupata madhara ya shambulio la moyo.

Amedai Ozoemena aliaguka wakati anatembea katika gereza hilo na alipopelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ndio ilibainika kuwa alipata shambulio la moyo na wakati akipatiwa matibabu alifariki dunia.

Wakili huyo amedai mteja wao alifariki wiki mbili zilizopita na tayari mwili wake umesafirishwa kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya mazishi.

Awali, Wakili wa Serikali Faraja Ngukah aliieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Ngukah baada ya kueleza hayo, wakili Yasini aliomba upande wa mashtaka kukamilisha haraka taratibu za kusajili taarifa na nyaraka muhimu Mahakama Kuu ili kesi hiyo iweze kuendelea.

"Mheshimiwa hakimu, kesi hii ni ya muda mrefu na washtakiwa wapo ndani hawana dhamana, hivyo ni vyema upande wa mashtaka wakafanya haraka kusajili taarifa muhimu Mahakama Kuu ili kesi hii iweze kuendelea kwa hatua nyingine," amedai wakili Yasini

Pia, wakili Yasin ameiomba siku kesi hiyo itakapoitwa mahakamani hapo, washtakiwa wapelekwe mahakamani ili waende kuonana na kiongozi wa Waendesha Mashtaka Mahakama ya Kisutu.

Akijibu hoja hizo, wakili Ngukah amedai atahakikisha nyaraka hizo zinasajiliwa mapema iwezekanavyo ili kesi hiyo hiyo iweze kuendelea.

Kuhusu hoja ya washtakiwa kueletwa mahakamani, wakili Ngukah amedai" Tutakapokamilisha kusajili nyaraka hizo, washtakiwa wataletwa mahakamani na kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo, hivyo sioni ulazima wa kuwaleta washtakiwa mahakamani hapa kwa kuwa wakili wao yupo hapa."

Hata hivyo, kesi hiyo imeendeshwa kwa njia ya video conference huku washtakiwa wakiwa mahabusu.

Hakimu Ngimilanga baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha mapema kusajili nyaraka hizo ili kesi iweze kuendelea kwa kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ngimilanga ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 13, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wapo gerezani kutokana na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Itakumbukwa kuwa April 7, 2021 washtakiwa hao walisomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo (Commital Proceedings) baada ya upelelezi wake kukamilisha, lakini baadaye kesi hiyo ilifutwa na kufunguliwa nyingine yenye mashtaka kama hayo.

Katika mashtaka yao, Linda anadaiwa Aprili 17, 2019, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam( JNIA), alikutwa akisafirisha dawa za kulevya ndani ya mabegi mawili yenye rangi ya brouni na nyeusi, moja lina kilo 15.8 na lingine kilo 4.8 za Heroine.

April 19, 2019 alikamatwa Plavins eneo la Kariakoo Dar es Salaam na alikiri kumsafirisha Linda kutoka Lativia kuja Tanzania kuchukua dawa hizo za kulevya na walikuwa wakiishi wote King's Hotel.

Muda mfupi baadaye, alikamatwa, Ozoemena na katika mahojiano na jeshi la polisi alikiri kumpatia Linda begi moja lilikuwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 15.8, wakati walipokutana na Plavins hotelini.

Mbali shtaka la kusafirisha dawa za kulevya, Ozoemena anakabiliwa na shtaka la kuishi nchini bila kuwa na kibali kwani aliingia nchini Julai mosi, 2017 na wakati anakamatwa kibali chake cha matembezi kilikuwa kimeisha muda mrefu.

Mwananchi
 
Kaenda kuzikwa kwao? Isijekuwa amejiangusha na kuchonga na madaktari.

NB: Habari sijaisoma kwa undani sana
 
Back
Top Bottom