Dar: Meli yenye magari 3,743 yawasili bandarini ikitokea Japan

Durban port







Port ya Taifa


Watanzania tunahitaji bandari kubwa kuliko hiyo ya Durban, tuna faida kubwa ya kijiografia kuzungukwa na 6 zisizo na bandari kabisa.

Beira Mozambique
 
Hapa nauona na kuushangaa utukufu wa mtu mweupe kwa kutengeneza hilo dubwana.TPA hawana maajabu yoyote.
 
Lakini unapotoka tu mbele na kusema "Mchina anataka asamehewe kodi" ni rahisi sana wananchi kuamini kwamba kumbe zile VAT, Import Tax, Excise Duty n.k zote hizo zinaenda kwa Mchina; jambo ambalo si kweli!!
Asante sana kwa kuniweka sawa. Bahati iliyoje baada ya kurudia tena kusoma posts ulizonijibu nimejua sasa kumbe mktaba haukuwepo, bali ilikuwepo framework of agreement. Na hii agreement imeisha expire.

Kwa hiyo siyo valid inatakiwa itupwe jalalani. Sasa, ili kukata kiu yangu na wengine ya kuongeza uelewa, unaweza kutusaidia kupata nakala ya hiyo expired framework of agreement kabla hawajaitupa jalalani? Hii itasaida kumkoma nyani giladi walio sema mradi ni mradi wa win-loose na wale wa win-win.

Natanguliza shukrani.

Hapa umenishauri nitafakari peke yangu. Nimefanya hivyo.
 
Ndio series yake yapo 11 EVER GREEN halafu bado kuna MAERSK nae ana vyuma bandari ya bongo haziingii
Du.... Kumbe ni balaa...

Kumbe tusianze kujisifu mapema... Bado madude yenyewe hayajatia nanga....
 
Meli imetoka mombasa kuja dar
Kwenye maelezo tunaongopewa imetoka japan moja kwa moja dar.....
 
Du.... Kumbe ni balaa...

Kumbe tusianze kujisifu mapema... Bado madude yenyewe hayajatia nanga....
Na hayatatia nanga kamwe kwa ufupi wa kina chetu cha maji na mlango wa kuingilia ni mdogo
 
Bandari Ina changamoto sana kiutendaji kuanzia storage facility, handling equipment, parking na system.

Humu Kuna raia Wana thubutu kulinganisha Dar Port na Durban Port
Wana wazimu hao.......bandari ya bongo inaendeshwa kilocal zaidi na sio kimataifa.....international
 
Halafu wanakwambia Bagamoyo ni mradi wa kishenzi, Kuna watu tutakufa tutaacha nchi bila kuwa na bandari kama ya Durban au hata Lamu ya 254
Niliona picha ya bandari ya bagamoyo ile ndio yenyewe sasa kimataifa zaidi
 
Mdau iyo meli imetumia shift nne kuimaliza magari yote 3743
 
Mnaosema bandari ya Dar haiwezi himili meli kubwa uongo wenu umeanza kuonekana
Maerks wana meli zinabeba tani 40,000 na zaidi. Kuna meli kibao zinabeba kontena zaidi ya 20,000 tena zinaenda meli kumi bandari moja. Wewe unakuja sema meli ya magari 3,000 tena moja kwa bandari nzima
 
Mdau iyo meli imetumia shift nne kuimaliza magari yote 3743
Mkuu performance tunacheki masaa/siku ukisema shift 4 maana yake ni masaa 33 na dakika 20 au siku 1 na masaa 9 dakika 20.

Kiutendaji tunaanza kuhesabu muda gari la kwanza lilipotoka na muda gari la mwisho lilipomaliza kushuka melini. Ndani ya shift 4 Kuna muda kazi ilikuwa inasimama (delays) huo muda lazima utolewe na ujulikane ndipo tunapata muda sahihi kazi ilipofanyika.

Mpaka muda nasoma sms Yako saa 1610HRS Local Time, hapa kwenye simu yangu nimetrack naiona hiyo meli bado ipo Bandari
 
Sisi wananchi wagonga ulimbo tunafaidikaje kuwasili kwa meli hiyo?
 
Siku moja nitaenda kutalii bandarini, nione hizo meli zinavyofanana, kwa kweli sikuwahi kufikiri kama meli inaweza kubeba magari mengi kiasi hicho
Mimi nilisikia meli inabeba makontena elfu16 nikabaki kushangaa tu
 

brother unazijuwa feeder vessels
 
Habari nzuri sana,haya ndio maendeleo,yasiohitaji tochi,tunayaona kwa macho yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…