Dar miaka ya nyuma ilikuwa tamu sana

Dar miaka ya nyuma ilikuwa tamu sana

Billicanas
California Dreamer
Fm club.... kwa macheni...
Good old days
 
Dar ya sasa ikoje kwani?
Dar ya sasa haina raha mkuu. Kulikuwa na raha miaka hiyo mkuu. Hadi uswazi ilikuwa full shangwe. Enzi hizo hata pale nyuma ya ikulu pale feri tulikuwa tunaenda kupunga upepo na watoto, lakini sasa hivi pamezibwa.
 
Ukiwa na pesa za kutosha hata Kama uko chato utaona Kama uko Los Angeles........tafuta pesa mkuu naona kwasasa unaandamwa na ukata, zerizi no wei utauona huu mji mtamu ukiwa "mgaa gaa na upwa".
 
Kweli Tz hatuwez kuwa super power......kwa thread kama hiz
 
Ukiwa na pesa za kutosha hata Kama uko chato utaona Kama uko Los Angeles........tafuta pesa mkuu naona kwasasa unaandamwa na ukata, zerizi no wei utauona huu mji mtamu ukiwa "mgaa gaa na upwa".
Kwa hiyo mkuu sehemu kama mambo club, billcanas club, mango garden, steers and debonears pizza and the like zimekufa kwa sababu mimi sina hela?
 
Dar ya sasa ikoje kwani?
Kweli dar hii hainogi nenda posta utakuta mtu anakaanga mihogo kwa kuni opposite na bank.vibanda vya machinga hadi karibu na ikulu,zamani kwenda posta unatafuta pamba kali sio siku hizi wanaenda posta na madera
 
Nakumbuka miaka ya 2001 kuja mpaka 2014 hivi Dar ilikuwa tamu mno. Maeneo ya Sinza na Mwenge ilikuwa maeneo matamu sana kuishi. Dah! Jamani Sinza ilikuwa tamu balaa, watoto wa Sinza walikuwa wakali balaa, hata sehemu zingine za uswazi nako watoto walikuwa wazuri balaa ila Sinza ndio ilikuwa maeneo matamu sana kuishi. Yaani ukisimama kwenye vituo vyote vya Sinza watoto wanaokuja kupanda daladala kwenda maeneo mbalimbali walikuwa wazuri balaa. Njoo posta mpya kipindi cha jioni watu wanaposubiria daladala kurudi nyumbani utafurahi mwenyewe maana wadada wote walikuwa warembo. Hadi watoto wa shule za sekondari wa enzi hizo walikuwa warembo hatari. Nakumbuka enzi hizo mambo ya internet kafee ndio yalikuwa yamepamba moto. Ukitaka kutuma email lazima uende internet cafe, basi huko full kupishana na watoto wazuri. Enzi hizo watoto walikuwa wanapenda sana miziki ya kimarekani, vijana wote walikuwa na swaga za kimarekani. Miziki kama in the club, dilema, babe boy na nyingine nyingi ilikuwa inabamba kweli. Bongo flavor nayo ilikuwa at its peak. Wakina Juma nature na songi la ugali na sonia, Ferouz na nyimbo yake ya starehe, mwana FA, Ray c, Gangwe mob, uswahilini matola na wengine wengi walikuwa the talk of the town. Siku ya Valentine barabarani kila mtu na mtu wake, wamevalia nguo nyekundu. Enzi hizo mapenzi hayakuwa ya kitapeli kama sasa hivi. Bar zilikuwa zinafurika kuanzia asubuhi, watu walikuwa na pesa, watu walikuwa wanatumia pesa. Asilimia kubwa ya wakazi wa Dar walikuwa na furaha, sio sasa hivi kila mtu ana majonzi ya ukata. Jamani zamani Dar ilikuwa tamu sana. Zamani Dar ilikuwa tamu sana.
Ni umri tu (those old good days) hakuna kilichobadilika
 
Ni umri tu (those old good days) hakuna kilichobadilika
Sidhani mkuu. Vitu kibao vilivyokuwepo enzi hizo havipo kwa sasa. Pale Ubungo mkabala na stendi ya daladala ya zamani kulikuwa na bar moja inaitwa Yenu bar, ilikuwa inabamba kinoma lakini sasa hivi haipo kabisa. Pia eneo hilo la Ubungo lilikuwa limechangamka sana, kulikuwa na mishemishe za hatari, watoto wa chuo walikuwa kama wote maeneo hayo. Kulikuwa na maduka na vimigahawa vingi. Huu ni mfano mmoja tu, maeneo mengi sana Dar yalikuwa full shangwe. Maeneo kama ya Sinza Kijiweni, Vatican, sinza kwa Remy, mapambano, madukani, kote huko kulikuwa raha tu.
 
Wakati huo ulikuwa 20s na sasa 30s hiyo ndiyo tofauti kwani unaona vitu tofauti. Walio katika 20s wanaona Dar ni moto. Waulize akina Salary Slip
 
Mademu wote walikua wanatafuta vyumba vya kupanga Sinza.
Mshkaji anakuaga anakwambia naenda kula mchemsho Sinza Mori au Africa sana.kipindi icho mchemsho umebamba ndo habari ya mjini.
 
Mademu wote walikua wanatafuta vyumba vya kupanga Sinza.
Mshkaji anakuaga anakwambia naenda kula mchemsho Sinza Mori au Africa sana.kipindi icho mchemsho umebamba ndo habari ya mjini.
Kabisa mkuu, kumbe na wewe unakumbuka utamu wa enzi hizo.
 
Dar ya sasa ni tamu zaidi, hata wasio na pesa wanatamba.
 
Ni jana tu nilikuwa naongea na Mrembo mmoja kuhusu raha zilizokuwepo Dar na sasa hivi ni DOROOOOO. Washamba toka maporini noma sana wameiharibu kabisa Dar kwenye Dept ya kujirusha na furaha sasa imebaki DOROOOOOO!
Hata Mimi nilitaka kumweleza Kama ulivyoeleza ila kwa maneno yangu.
Kuwa,wakati huo nchi ilikua inaongozwa na watoto wa mjini,na Dar Ni sehemu ya nchi hii.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom