Dar miaka ya nyuma ilikuwa tamu sana

Billicanas
California Dreamer
Fm club.... kwa macheni...
Good old days
 
Dar ya sasa ikoje kwani?
Dar ya sasa haina raha mkuu. Kulikuwa na raha miaka hiyo mkuu. Hadi uswazi ilikuwa full shangwe. Enzi hizo hata pale nyuma ya ikulu pale feri tulikuwa tunaenda kupunga upepo na watoto, lakini sasa hivi pamezibwa.
 
Ukiwa na pesa za kutosha hata Kama uko chato utaona Kama uko Los Angeles........tafuta pesa mkuu naona kwasasa unaandamwa na ukata, zerizi no wei utauona huu mji mtamu ukiwa "mgaa gaa na upwa".
 
Kweli Tz hatuwez kuwa super power......kwa thread kama hiz
 
Ukiwa na pesa za kutosha hata Kama uko chato utaona Kama uko Los Angeles........tafuta pesa mkuu naona kwasasa unaandamwa na ukata, zerizi no wei utauona huu mji mtamu ukiwa "mgaa gaa na upwa".
Kwa hiyo mkuu sehemu kama mambo club, billcanas club, mango garden, steers and debonears pizza and the like zimekufa kwa sababu mimi sina hela?
 
Dar ya sasa ikoje kwani?
Kweli dar hii hainogi nenda posta utakuta mtu anakaanga mihogo kwa kuni opposite na bank.vibanda vya machinga hadi karibu na ikulu,zamani kwenda posta unatafuta pamba kali sio siku hizi wanaenda posta na madera
 
Ni umri tu (those old good days) hakuna kilichobadilika
 
Ni umri tu (those old good days) hakuna kilichobadilika
Sidhani mkuu. Vitu kibao vilivyokuwepo enzi hizo havipo kwa sasa. Pale Ubungo mkabala na stendi ya daladala ya zamani kulikuwa na bar moja inaitwa Yenu bar, ilikuwa inabamba kinoma lakini sasa hivi haipo kabisa. Pia eneo hilo la Ubungo lilikuwa limechangamka sana, kulikuwa na mishemishe za hatari, watoto wa chuo walikuwa kama wote maeneo hayo. Kulikuwa na maduka na vimigahawa vingi. Huu ni mfano mmoja tu, maeneo mengi sana Dar yalikuwa full shangwe. Maeneo kama ya Sinza Kijiweni, Vatican, sinza kwa Remy, mapambano, madukani, kote huko kulikuwa raha tu.
 
Wakati huo ulikuwa 20s na sasa 30s hiyo ndiyo tofauti kwani unaona vitu tofauti. Walio katika 20s wanaona Dar ni moto. Waulize akina Salary Slip
 
Mademu wote walikua wanatafuta vyumba vya kupanga Sinza.
Mshkaji anakuaga anakwambia naenda kula mchemsho Sinza Mori au Africa sana.kipindi icho mchemsho umebamba ndo habari ya mjini.
 
Mademu wote walikua wanatafuta vyumba vya kupanga Sinza.
Mshkaji anakuaga anakwambia naenda kula mchemsho Sinza Mori au Africa sana.kipindi icho mchemsho umebamba ndo habari ya mjini.
Kabisa mkuu, kumbe na wewe unakumbuka utamu wa enzi hizo.
 
Dar ya sasa ni tamu zaidi, hata wasio na pesa wanatamba.
 
Ni jana tu nilikuwa naongea na Mrembo mmoja kuhusu raha zilizokuwepo Dar na sasa hivi ni DOROOOOO. Washamba toka maporini noma sana wameiharibu kabisa Dar kwenye Dept ya kujirusha na furaha sasa imebaki DOROOOOOO!
Hata Mimi nilitaka kumweleza Kama ulivyoeleza ila kwa maneno yangu.
Kuwa,wakati huo nchi ilikua inaongozwa na watoto wa mjini,na Dar Ni sehemu ya nchi hii.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…