Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mgombea Urais kupitia Chama Cha ACT Wazalendo Luhaga Joelson Mpina, leo Jumamosi ya Septemba 13, 2025 amefika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi(INEC) zilizopo Posta, jijini Dar es Salaam Kwa ajili ya kurudisha fomu yake ya kugombea Urais.
Mpina akiwa na Mgombea Mwenza Bi. Fatma Fereji wamerejesha fomu hiyo baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma uliotoka Septemba 11, 2025 kuwa mchakato wa kurudisha fomu ya Mpina uendelee kutokana na kile kilichoelezwa kuwa utaratibu wa kumzuia kurejesha fomu awali haukuwa sahihi.
Wagombea hao wameambatana na viongozi waandamizi wa chama chao akiwemo Kiongozi wa Chama Dorothy Semu, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Omar Shaaban, Sheikh Ponda Issa Ponda ambae ni mgombea ubunge wa jimbo la Temeke na Naibu Katibu wa Uenezi Taifa Shangwe Ayo.