Kwa wale wafuatiliaji wa mambo, siku kadhaa zilizopita chaneli ya DAR MPYA ilipata misukosuko kidgo na TCRA baada ya kuchapisha maudhui yaliyoonesha baadhi ya watu "waliodaiwa" kupangwa ili kufanya propaganda kuhusiana na suala zima la Ngorongoro.
Pamoja na misukosuko hiyo, mapema mwezi wa saba, DAR Mpya waliandika katika ukurasa wao wa Twitter wakisema kwamba wamefutiwa mashtaka na kamati ya maudhui ya TCRA lakini wametakiwa kuhuisha leseni yao haraka iwezekanavyo.
Lakini usiku huu, dakika kadhaa zilizopita, Chaneli hiyo ya mtandaoni imeandika tena katika ukurasa wake wa Twitter imesema kwamba kuanzia sasa itaanza kuitwa ZAMAMPYA ONLINE TV. Je. Tusahau kuhusu DAR MPYA ONLINE TV ama nini?