JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mtoto Patrick Dickson ambaye alipotea kwao kwa siku kadhaa mwanzoni mwa mwezi huu Mei 2022 amepatikana na kusimulia kuwa alikuwa akitumikishwa katika kazi ya kuombaomba mtaani pamoja na kuvutishwa sigara.
Mtoto huyo ambaye alipatikana Mei 23, 2022 amesema: “Siku ya kupotea kwangu nilitoka nyumbani kwenda kucheza sikwenda shule, nikarudi usiku saa moja mama akajua kuwa nilimdanganya, akanichapa nikatoroka kwenda Kariakoo.
“Huko nikakutana na watoto wenzangu, nikawa nashinda nao, kuna mdada tulikutana naye akanichukua, baadaye kuna mwanaume alikuja kwa huyo mdada akanichukua nikawa naishi naye.
"Akanichukua awaka ananitumikisha kazi, akawa anatupeleka mtaani kuomba hela, tukirudi jioni tunampa hela yeye, akawa anatuvutisha sigara, niliwahi kujaribu kutoroka akanikamata akanipiga.
“Nilipotoroka tena nikaenda Bunju ndio kuna wenzangu wakubwa wakanirudisha nyumbani.”
Mama wa mtoto huyo Martha William amesema walitoa taarifa Polisi pamoja na kwenye kituo cha ITV juu ya kupotea kwa mtoto huo na anashukuru amerejea salama.
Chanzo: ITV