TANZIA Dar: Pacha Rehema aliyebaki baada ya kutenganishwa naye afariki dunia

TANZIA Dar: Pacha Rehema aliyebaki baada ya kutenganishwa naye afariki dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
FWaAS9kXoActJKm.jpg

Mtoto Rehema ambaye ni pacha aliyekuwa amesalia baada ya mwenzake waliyetenganishwa kufariki dunia, naye ameaga Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana Agosti 11, 2022.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema: "Ni kweli amefariki jana saa tano asubuhi".

Watoto hao walifanyiwa upasuaji wa kutenganishwa Julai Mosi, 2022, pacha wa kwanza, Neema alifariki Julai 10, 2022.

Pia soma:
Pacha waliotenganishwa, mmoja afariki dunia
 
Pole kwa wafiwa.

Madaktari wasivunjike moyo, hata mbuyu ulianza kama mchicha, ni kweli kibinadamu inaumiza kuna watu watahisi madaktari wanachezea uhai wa watu.

Ila hakuna mafanikio bila majaribio kadhaa yaliyoshindikana, inaumiza tu kwa kuwa ni binaadamu mwenzetu, hata huko kwa wenzetu yanatokea, si kila wanalofanya wanafanikiwa.

Watanzania tujifunze kupunguza lawama, tunawavunja moyo watu wanaojaribu kutafuta namna ya kutuponya hapa hapa nchini.
 
Mloganzila university teaching hospital tuleteeni wanatalaluma kutoka EUROPE and AMERICA waje wafundishe madactari nchini.
 
Madaktari walifanyia majaribio hawa watoto... Kitendo cha yule wa kwanza kufa ndani ya siku 14 ilikua ni ishara operation ilikua ya mchongo...
 
Pole kwa wafiwa.

Madaktari wasivunjike moyo, hata mbuyu ulianza kama mchicha, ni kweli kibinadamu inaumiza kuna watu watahisi madaktari wanachezea uhai wa watu.

Ila hakuna mafanikio bila majaribio kadhaa yaliyoshindikana, inaumiza tu kwa kuwa ni binaadamu mwenzetu, hata huko kwa wenzetu yanatokea, si kila wanalofanya wanafanikiwa.

Watanzania tujifunze kupunguza lawama, tunawavunja moyo watu wanaojaribu kutafuta namna ya kutuponya hapa hapa nchini.
Unataka tuwatie moyo kwa uzembe wa wazi na makusudi kabisa..? Waliwafanyia operation kwajil yakutaka sifa tu, ilitakiwa wangoje watoto wakomae kidogo... Baadhi ya madaktari walihojiwa kabla ya operation, wakasema kisomi zaidi wanatakiwa wafanyiwe baada ya mwaka au miaka miwili...
 
Mloganzila ni Tawi la chuo cha mhimbili na sio hospital...uhaba wa hospitali unaifanya kuwa hospital. Ukipelekwa mloganzila na issue nyeti, 50/50 kupona
 
Pole kwa mama mfiwa,Madakatari mjitathmini,siku nyingine watu wataogopa kutenganisha watoto sasa
sasa wangekuaje wakiwa hivyo jaman! kumbuken hiyo operationa yao walikuwepo na wazungu kibao hapo! Imeandikwa hivyo tu jaman maisha ni kubahatisha
 
Back
Top Bottom