TANZIA Dar: Pacha Rehema aliyebaki baada ya kutenganishwa naye afariki dunia

Umeandika vema, lakini tuna madaktari hapa Tanzania nadhani hizo lawama zinawahusu,, mimi ni mhanga wa moja wa madaktari hao.. Afya imekua biashara na sio huduma tena
 
Wangewaacha tu pengine wangeishi maisha marefu tu kama wale Maria na Consolata.

Mbwembwe kibao,makamera chumba cha upasuaji na battalion ya mabingwa room imefulika km Simba day.
 
Trials + Errors=Perfect
 
Katika ya sekta ya afya, idara iliyo nyuma sana ni clinical care baada ya operation.

Hapo ina maanisha clinical service, nursing na kwa ujumla uangalizi wa mgonjwa baada ya operation.
Hapa Tanzania tuko nyuma sana.

Ni heri hao watoto wangetenganishwa na kubaki India.
 
RIP Pacha. Hivi Madaktari wa bongo wamesomea nn?
No, tusianze kuwalaumu madaktari wakati hatujui muunganiko wa watoto hao ulikuwaje. Yawezekana kulikuwa na utata (complication).
 
Taarifa mbaya kabisa hii.

Apumzike kwa amani binti yetu
 
No, tusianze kuwalaumu madaktari wakati hatujui muunganiko wa watoto hao ulikuwaje. Yawezekana kulikuwa na utata (complication).
Kama kulikua na utata why walifanyiwa operation?huwezi aka bet kwenye uhai wa binadamu, nchi zinazojielewa permits za madakitari hawa zingesimamishwa hadi tume huru ya wataalamu ije na mrejesho, huyu mama mfiwa iM sorry hakuna kitakachofanyika kwake, Angelus kwenye nchi zinazojielewa ,angemfungulia kesi ya madai waziri wa afya, hospital iliyo fanya operation hii,na madakitari, but bongo land hawa doctors maisha yao yanaendelea Maana wao na familia zao ni matibabu UK,India, US au Millpark med clinic
 
Tangu awali binafsi nilisema kutenganishwa na kufanikiwa kwa iparesheni ni mambo mawili tofauti, hats hivyo haukupita muda mmoja alifariki na sasa huyu naye amefariki!, pole mama mzazi wa mapacha hawa.
 
Wenzetu nchi zile juzi tu wametenganisha watoto walioungana ubongo! Sisi bado sanaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…