Mkuu hayo maeneo mengi ya wazi unayosema ni yepi?
Naomba yataje baadhi!
Halafu huwa inategemeana na convenience ya Mtu , mfano mwingine atokapo kazini jioni huwa anarudi nyumbani Kwa njia ya Mazoezi !
Na makazi ya watu yametawanyika!
Nitajie Public Gaderns Za Mazoezi Kama zipo!
Mkuu kila kitu kinapaswa kufanywa kwa wakati na mahali pake. Mazoezi kama sehemu nyingine yoyote ya shughuli za kila siku zinapaswa zifanywe katika maeneo elekezi
Ni kweli serikali inataka tufanye mazoezi.. Ila hamaanishi tusifuate utaratibu. Ili kukusanyika kwa namna yoyote ile na kundi ni kubwa tunahitaji kutoa taarifa.. Ili mamlaka zifahamu.
Lakini pia kwa hao wanakusanyiko kuna dharura.. Ajali nk ikiwa mamlaka zinajua inakuwa na uhaisi wa kupata msaada Wa dharura unapohitajia na mamlaka zinakuwa zinajua tentatively zinadeal na kundi kubwa kiasi gani
Tukirejea kwenye mazoezi ..wanasayansi wanakubaliana nami naposema kufanya mazoezi katika njia kuu za magari ni hatari kwa afya yako.. Mwili wako wakati wa mazoezi unahitaji hewa nyingi zaidi na mbaya ni kuwa hewa inayokuzunguka kwa wakati upo barabarani so hewa salama inapochangamana na moshi wa motokaa.
Kweli tunataka kuboresha afya za watanzania ila ni lazima kama serikali tuzijali pia. Tumepata taarifa itakayosaidia maboresho tunaifanyika kazi.. Maana serikali inawapenda watu wake.
Hatari zingine ni pamoja na ajali..zinazoweza kutokea wakati wa maandamano haya ya kimichezo.. Utayari wao kukabiliana na hatari hizi ..je kindi moja Liwe na ukubwa gani?! Ni baadhi ya concern tunazopaswa kuzijua ili kuepusha majanga huko mbeleni.
Kwa Kamanda wetu anayo haki ya kuwatetea watumiaji wa barabara .. Kwa kujua kwake taarifa kama ukubwa na kundi, muda utakaotumika kupitia Barabara zetu, barabara gani zitatumika.. Anapata wasaa wa kupangilia na kusimamia Magari na waenda kwa miguu hawa na wakati mwingie anaweza kuwapa alternative routes zinakazo punguza usumbufu kwa watumiaji wa magari na hawa waenda kwa miguu.
Swali lako LA viwanja naomba niseme.. Viwanja vipo viiiingi sana .. Kuna fukwe nyiiingi sana.. Karibia kila shule ya msingi inavyoviwanja.. Shule za sekondari zinavyo viwanja.. Tuanzie hapo. Kila mtu asogee shule ya msingi uliyopo karibu yake.
Lakini kama unaona huko hapakubariki basi sogea viwabja vya zakhiem, kibasila, uwanja wataifa, mchicha Kule kupita reli kama ubaenda kwa limboa vipo viwanja.. Panga gari njoo mpaka Pwani ya Aghakhan , Coco, leaders, Biafra, shule ya msingi Magomeni, mlimani na Ardhi university, viwanja vya posta kijitonyama, huko ubungo ndo mapori kila kona.. Mazoezi mfanye tu hata kwako nyumbani inawezekana.
Tukianzia huko mkuu.. Hayo maeneo tunaanza kuuona umuhimu wake yaliyoibwa tutayadai.. Na tunakoenda kuanzisha makazi mapya tutayaweka yaliyobora zaidi. Kwa mapungufu tutayaona na tutaanza kuyarekebisha.
Wasalaam