Dar: RC Makalla atembelelea Masoko ya Simu 2000 na Mahakama ya ndizi Mabibo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
*RC MAKALLA AFANYA MAAMUZI MAGUMU, AAGIZA MABORESHO YA KWANZA SOKO LA SIMU 2000 NA SOKO LA MABIBO

- Asema hoja Za Wafanyabiashara zina uzito hivyo waboreshewe kwanza kisha kamati ya soko Na serikali wakae kupendekeza vibanda uniform rafiki kwa wafanyabiashara.

- Wafanyabiashara wapongeza uamuzi wa Mkuu wa Mkoa baada ya awali kukataa mpango wa Manispaa wa kuwajengea shades badala ya Vibanda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuhakikisha maboresho ya kwanza kwenye Soko la simu 2000 yanafanyika kwa kuzingatia Maoni yaliyopendekezwa na Wafanyabiashara wa Soko Hilo.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kusikiliza kero kwenye Soko Hilo ambapo amesema Maoni na mapendekezo yote Tisa ya Wafanyabiashara ni vizuri yakazingatiwa kwakuwa kila mmoja ameonekana kuwa na hoja za Msingi kulingana na Aina ya Biashara anayofanya.

Hatua hiyo imekuja Mara Baada ya Serikali kutoa fedha za kuboresha Soko lakini Aina ya michoro/ Design za Ujenzi wa vibanda/shade zilizopendekezwa na Serikali imeonekana kuwa rafiki kwa baadhi ya Biashara na wakati huohuo kuonekana sio rafiki kwa biashara nyingine.

Kutokana na mkanganyiko huo, RC Makalla ameelekeza Kamati ya Soko iliyoundwa kukaa kwa pamoja na kupitia upya mapendekezo ya Wafanyabiashara ili yaweze kufanyiwa kazi.

Aidha RC Makalla ameelekeza LATRA kuongeza route za Daladala, DAWASA kufikisha huduma ya Maji sokoni hapo, TANESCO kushughulikia huduma ya umeme na TARURA kuhakikisha inaboresha Miundombinu ya Soko.

Katika ziara ya RC Makalla amepokea kero na changamoto mbalimbali ambapo zote kwa pamoja ameahidi zitatatuliwa kwa haraka.

Kwa upande wao baadhi ya Wafanyabiashara Wamemshukuru RC Makalla kwa uamuzi wake wa kuwatembelea na kutatua kero na changamoto zao zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu ambapo wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali sikivu ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla leo amefanya ziara kwenye Soko la Mabibo maarufu Kama Mahakama ya ndizi ambapo amewahakikishia Wafanyabiashara wa Soko Hilo kuwa Serikali haina Mpango wa kubadili umiliki wa Soko Hilo Bali amekwenda kutatua kero zilizopo sokoni hapo ili biashara zifanyike pasipo usumbufu.

RC Makalla amesema hayo alipofanya ziara sokoni hapo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutatua kero na changamoto za Wananchi ambapo baadhi ya Wafanyabiashara walihisi huenda Serikali imekwenda kubadili umiliki wa Soko Hilo ambalo lilirejeshwa kwa Wafanyabiashara na Hayati Rais Magufuli mnamo mwaka 2020.

Akiwa sokoni hapo RC Makalla amepokea Kilio Cha Wafanyabiashara kuhusu Ufanyaji biashara holela nje ya Soko na kusababisha wale Wanaofanya biashara kwenye maeneo waliyopangwa kukosa wateja ambapo amepiga marufuku Ufanyaji Biashara nje ya masoko kwakuwa imekuwa ikisababisha Masoko kufa.

Aidha RC Makalla amepokea changamoto ya ubovu wa Miundombinu ya Soko ambapo ameelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na uongozi wa Soko kufanyia kazi changamoto hiyo.

Pia soma:

Thread 'Hali ya soko la Mabibo wakati wa mvua ni mbaya sana' Hali ya soko la Mabibo wakati wa mvua ni mbaya sana
 
*RC MAKALLA AFANYA MAAMUZI MAGUMU, AAGIZA MABORESHO YA KWANZA SOKO LA SIMU 2000 NA SOKO LA MABIBO

- Asema hoja Za Wafanyabiashara zina uzito hivyo waboreshewe kwanza kisha kamati ya soko Na serikali wakae kupendekeza vibanda uniform rafiki kwa wafanyabiashara.

- Wafanyabiashara wapongeza uamuzi wa Mkuu wa Mkoa baada ya awali kukataa mpango wa Manispaa wa kuwajengea shades badala ya Vibanda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuhakikisha maboresho ya kwanza kwenye Soko la simu 2000 yanafanyika kwa kuzingatia Maoni yaliyopendekezwa na Wafanyabiashara wa Soko Hilo.

RC Makalla
ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kusikiliza kero kwenye Soko Hilo ambapo amesema Maoni na mapendekezo yote Tisa ya Wafanyabiashara ni vizuri yakazingatiwa kwakuwa kila mmoja ameonekana kuwa na hoja za Msingi kulingana na Aina ya Biashara anayofanya.

Hatua hiyo imekuja Mara Baada ya Serikali kutoa fedha za kuboresha Soko lakini Aina ya michoro/ Design za Ujenzi wa vibanda/shade zilizopendekezwa na Serikali imeonekana kuwa rafiki kwa baadhi ya Biashara na wakati huohuo kuonekana sio rafiki kwa biashara nyingine.

Kutokana na mkanganyiko huo, RC Makalla ameelekeza Kamati ya Soko iliyoundwa kukaa kwa pamoja na kupitia upya mapendekezo ya Wafanyabiashara ili yaweze kufanyiwa kazi.

Aidha RC Makalla ameelekeza LATRA kuongeza route za Daladala, DAWASA kufikisha huduma ya Maji sokoni hapo, TANESCO kushughulikia huduma ya umeme na TARURA kuhakikisha inaboresha Miundombinu ya Soko.

Katika ziara ya RC Makalla amepokea kero na changamoto mbalimbali ambapo zote kwa pamoja ameahidi zitatatuliwa kwa haraka.

Kwa upande wao baadhi ya Wafanyabiashara Wamemshukuru RC Makalla kwa uamuzi wake wa kuwatembelea na kutatua kero na changamoto zao zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu ambapo wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali sikivu ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla leo amefanya ziara kwenye Soko la Mabibo maarufu Kama Mahakama ya ndizi ambapo amewahakikishia Wafanyabiashara wa Soko Hilo kuwa Serikali haina Mpango wa kubadili umiliki wa Soko Hilo Bali amekwenda kutatua kero zilizopo sokoni hapo ili biashara zifanyike pasipo usumbufu.

RC Makalla amesema hayo alipofanya ziara sokoni hapo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutatua kero na changamoto za Wananchi ambapo baadhi ya Wafanyabiashara walihisi huenda Serikali imekwenda kubadili umiliki wa Soko Hilo ambalo lilirejeshwa kwa Wafanyabiashara na Hayati Rais Magufuli mnamo mwaka 2020.

Akiwa sokoni hapo RC Makalla amepokea Kilio Cha Wafanyabiashara kuhusu Ufanyaji biashara holela nje ya Soko na kusababisha wale Wanaofanya biashara kwenye maeneo waliyopangwa kukosa wateja ambapo amepiga marufuku Ufanyaji Biashara nje ya masoko kwakuwa imekuwa ikisababisha Masoko kufa.

Aidha RC Makalla amepokea changamoto ya ubovu wa Miundombinu ya Soko ambapo ameelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na uongozi wa Soko kufanyia kazi changamoto hiyo.

Pia soma:

Thread 'Hali ya soko la Mabibo wakati wa mvua ni mbaya sana' Hali ya soko la Mabibo wakati wa mvua ni mbaya sana
Kumbe na yeye alianza na style ya kutembelea masoko.
 
Back
Top Bottom