Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Kosa kubwa la Polisi hapo ni lugha ya kibabe kwa mwanajeshi.Na hata huvyo asingeweza kutoa pesa katika ATM kwasababu ATM huwa aifanyikazi wanapokuwa wanaweka pesa.

Lugha ya kibabe ndo imewaponza Polisi.
Wewe nawe huwa unaleta mada za jela na kutetea watu kupekuliwa matako unashindwa kuelewa suala la wazi kama hili? Pale ishu siyo ATM kutoa pesa au kutotoa pesa, suala ni usalama wa pesa na maisha ya askari wanaosimamia hilo zoezi hilo, hapo ni UBABE, nasema tena ni ubabe unatakiwa kutumika pale, sio ombi wala kubembelezwa, ni amri, hivi mkuu kweli hujui kabisa kwamba amri ni ubabe?
 
Polisi hawataki kuwatii wanajeshi kuna sehemu unakuta hata Polisi hataki kumpigia Mwanajeshi Afisa salute mpaka akoromewe na Mwanajeshi.

Nakumbuka kuna siku tulikuwa tunasafiri tulifika mahali akapita Polisi na tulikuwa na Capten wa JWTZ yule Polisi Constable alipita tu kuna Surgent wa JWTZ tuliokuwa naye akamuita yule Polisi na kumuuliza huoni hapa kuna Afisa wa Jeshi ambaye anatakiwa kupewa heshima yake kwa kupigiwa Salute? Yule Polisi akaanza kujikanyaga kanyaga tu pale na kuomba samahani maana kilichokuwa kinafuata pale ni adhabu kwa yule Polisi kushindwa kutimiza matakwa ya kijeshi kwa Kupiga salute kwa Afisa yoyote anayekutana naye mbele yake bila kujali anatoka jeshi gani.
 
Jambazi hawezi kuiba pesa toka sehemu ya kutolea pesa kwenye ATM hata kama kule ndani wakiwa wanaweka.Hata kama angeingia kwenye ATM nothing could happen.

Nakumbuka hata yule kijana wa kiislam aliyeuwawa kule Kurasini ilikuwa hivyo hivyo yule kijana alikuwa na tatizo la kusikia kwahiyo hata alipokuwa anaambiwa na Polisi kuwa usiende huko hakuweza kusikia na hatimaye alipigwa risasi bila hata kuonyesha dalili ya kufanya uhalifu wowote.Weledi wa Polisi katika baadhi ya matukio bado unakuwa si mzuri sana
 
Sisi wengine tunajifanya hatuhusiki kumbe unafiki mtupi wote kwa umoja wetu tupaze sauti kukataa yasiyo ridhisha bila kujali anatendewa nani na wala nisijidanganye bure maana wote tunahusika
Tupaze sauti sababu ya mjeda asiyetaka kutii amri halali na kufuata maadili ya kazi yake?

Hata kama alivaa sare za jeshi bado tahadhari ilihitajika. Kuna wahalifu kibao wametumia sare za majeshi.

Pole kwa wafiwa na huyo mjeda lazima awajibike.
 
Polisi jeshi (MP)ni msimamizi wa sheria za kijeshi tu.
Kwenye makosa ya kiraia hahusiki nayo.
 
Hilo la mjinga na mwenye akili tuliache kwanza, ila alichofanya askari wa JWTZ ni aibu kwa jeshi, anatakiwa achukuliwe hatua, ila kulindana pia bado kupo, inaweza ikapotezewa kimya kimya au jeshi likamkana kuwa siyo mtu wetu, na kumficha mahali..
Jeshi halina utaratibu wa kulinda watu wajinga.

Mpaka sasa huyo ni mali ya polisi.
 
Kwa maoni yangu naona kosa lililopo ni kutotambuana, Laiti wangetambuana kusingetokea mabishano, Polisi angetambua mapema yule nae ni askari kusingekuwepo mabishano kwani wangeendelea na shughuli yao ya kuweka pesa pale ATM. Maana hata huyo mwanajeshi ni mwanausalama wetu. Na mwanajeshi hakupenda kutolewa kwa kauli hiyo ya kuondoka maana ingejulikana ni mwanajeshi na ameondolewa kizembe nadhani angefukuzwa kazi kwani angeonyesha udhaifu, Na huyo askari alishindwa kujiongeza kwa nn huyu mtu ni jasiri kiasi hiki? Mpaka yule kushika vile Bunduki hakutambua huyu ni askari. Mm niliona siku moja askari alikuwa anamhoji askari mwenzake lakini aling'amua na kumuacha aendelee na Safari zake
 
Kupitia hii thread...nimewajua wazee wa " Aroooo kuja hapa au nikupige virungu"
 
Nidhamu ya askari inajengwa mafunzoni. Kila mlinda usalama ana mipaka yake. Polisi akiwa kazini akakusimamisha pale haijalishi ni nani. Hivi kwa mfano FBI na CIA wanafanyiana ubabe wa kitoto hivi? Ugomvi unaweza kutokea kwa bahati mbaya lakini si mfumo huu unaonesha kuna dharau kati ya majeshi! Hili lisipuuzwe ...tuliona askari wa JWTZ wakimpiga Traffic ...sometimes askari wetu kupiga raia ovyo ....kwa ulimwengu wa sasa hili limepitwa na wakati! Mambo ya kuvamia mtaa kisa mwenzao kapigwa au kaibiwa? Mnapiga hadi wasiohusika? Si mtumie mbinu zenu kuwabaini na kudeal nao?
 
Kosa kubwa la Polisi hapo ni lugha ya kibabe kwa mwanajeshi.Na hata hivyo asingeweza kutoa pesa katika ATM kwasababu ATM huwa aifanyikazi wanapokuwa wanaweka pesa.

Lugha ya kibabe ndo imewaponza Polisi.
Hekima na busara inahitajika pande zote mbili,huyo mwanajeshi anaweza poteza kazi kwa uzembe wake mwenyewe kwa kushindwa kucontrol hasira zake,
 
Mimi siyo polisi na siwezi kuwa polisi, kuopen fire ovyo ovyo kivipi, askari anaona mwenzie anataka kupokonywa silaha afanyeje?, aangalie tu?

Hapo kwenye red..Haihitaji akili ya kurusha roketi kujua wewe ni nani . ?? Mbona ni rahisi sana..


Hapo kwenye bold Nyeusi....
Inamaana habari hujaisoma au...?? Au ndio kujitoa ufahamu sio..!!!??
Ilikuwa hivi
kulikuwa na askari wa JWTZ aliyekuwa akitaka kutoa pesa kwenye mashine
Halafu wakafanya hivi..

Kulwa alimfuata jamaa huyo akiwa na bunduki mkononi huku akimuelekezea
Mwanajeshi akafanya hivi..
mwanajeshi huyo aliikamata na kuelekezea mtutu juu, jambo lililoonekana kuwa alikuwa na utaalam wa masuala ya silaha.


Sasa hebu niambie hapo alitakaje kumpokonya silaha..

Au ndio Polisi mnatumia zile mbinu zenu kishenzi za kutwist ushahidi ili kujilinda...? Yani unataka kumbambika Mwanajeshi kesi ya uporaji..


Shame on you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…