[emoji3][emoji3]ahahahhaha mkuu nimeona hilo neno raia wa kawaida hawezi jua maana yake....
hahhaha mambo ya nua sio mchezo..
Wewe mwenyewe ni mbwa tu huna loloteDaaaah pole sana mwanajeshi na sijui kwanini hakumnyanganya kabisa ile bunduki na kulenga yule pimbi aliyekuwa amebaki kwenye gari nawachukia sana hawa mbwa wa kaki ***** zao narudia tena pole sana mwanajeshi Mungu akufanyie wepesi upone haraka
Hata wewe utakufa siku moja2Kwa hawa jamaa siwezi kusikitika kabisa na tena kama ingewezekana wangelipuana kikosi kwa kikosi
Watakuchakaza hiyo ilikua bahati mbaya tu. Ingekua hivyo usemavyo si ingekua wote wameisha?Jaribu kutumia akili kidogo hata km unawachukiaHii inaonyesha askari Polisi hawana mafunzo ya kutosha ya matumizi ya silaha. Ndio maana ni vituko tuu kama tulivyoona kwa Malima, kule Morogoro au hata kwa Akwilina
Utawezaje kutoa pesa ATM wakati wanaweka ,,, Elimu muhimu sana si kwa majeshi tu Bali kwa jamii nzima .
Nadhani hujaelewa, hao wawekaji wamemkuta anatoa pesa. Ingekuwa busara kumwambia maliza kutoa pesa na kadi yako usogee tuweke pesa basi!
Kifo cha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Konstebo Kulwa Gilbert, aliyepigwa risasi kwa bahati mbaya na mwenzake, kimezua mshtuko kwa ndugu, jamaa, askari wenzake na majirani aliokuwa akiishi nao nyumbani kwake, Ukonga-Mazizini jijini Dar, Gazeti la Uwazi pekee ndilo lenye mkasa mzima wa tukio hilo.
NI SINZA JIJINI DAR
Tukio hilo la kusikitisha lililotokea Jumanne ya wiki iliyopita, majira ya jioni wakati afande Kulwa na FFU wenzake wakiwa na askari wa kampuni binafsi ya ulinzi wakishusha pesa kwa ajili ya kuziweka kwenye mashine ya ATM ya Benki ya CRDB iliyopo Sinza-Mori pembezoni mwa Kituo cha Mafuta cha Big Bon, jijini Dar.
Mashuhuda wa tukio hilo waliliambia Uwazi kuwa, wakati maafande hao wakiwa kwenye harakati za kushusha pesa hizo karibu na mashine hiyo, kulikuwa na askari wa JWTZ aliyekuwa akitaka kutoa pesa kwenye mashine hiyo hivyo afande Kulwa na wenzake walimuamrisha aondoke haraka eneo hilo kwa sababu za kiusalama.
MASHUHUDA WASIMULIA
Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda hao, Jimmy Kaishozi, mkazi wa Sinza-Meeda, mwanajeshi huyo, baada ya kupewa amri ya kuondoka haraka eneo hilo, aliona kama amedharauliwa na askari hao hivyo aliwataka wamwambie kistaarabu na siyo kumwamrisha.
Kaishozi alisimulia kuwa, hali hiyo ilizua malumbano kati ya askari hao na mwanajeshi huyo ambapo Kulwa alimfuata jamaa huyo akiwa na bunduki mkononi huku akimuelekezea ambapo mwanajeshi huyo aliikamata na kuelekezea mtutu juu, jambo lililoonekana kuwa alikuwa na utaalam wa masuala ya silaha.
“Kitendo hicho kilizidisha taharuki ambapo askari mwingine wa FFU naye alitoka kwenye gari lililokuwa limebeba pesa na bunduki nyingine na kumlenga mwanajeshi huyo, lakini katika hali iliyoonekana kama bahati mbaya, risasi hizo zilimpata afande Kulwa na nyingine ilimlenga mwanajeshi huyo.
“Hapo mapambano yalizidi kukolea kama sinema ya kivita ambapo askari aliyekuwa akilenga shabaha, alipoona amempiga mwenzake, aliikoki tena bunduki na kumpiga risasi nyingine mwanajeshi huyo ambapo afande Kulwa na mwanajeshi huyo, wote walianguka chini na kuanza kutapatapa huku wakitokwa na damu nyingi.
“Ilichukua muda wakigaragara chini hadi walipofika askari wa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) na kuwachukua, sijui walipelekwa wapi,” alisimulia Kaishozi.
KITUO CHA MABATINI
Hata hivyo, habari kutoka Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) ambapo mwandishi wetu alifika, baadhi ya polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, wakisema kuwa majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wakiwa njiani afande Kulwa aliaga dunia.
MAKAO MAKUU FFU
Mwandishi wetu pia alikwenda Makao Makuu ya Kikosi cha Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), Ukonga-Madafu jijini Dar ambapo aliwakuta askari wenzake marehemu ambao walionesha hisia za majonzi wakati wakizungumzia kifo cha mwenzao huyo.
Askari hao hawakuwa tayari kuandikwa majina kwa maelezo kuwa hawaruhusiwi ambapo walimwelekeza mwandishi wetu nyumbani kwa marehemu Ukonga-Mazizini jijini Dar.
NYUMBANI KWA MAREHEMU
Mwanahabari wetu alifika nyumbani kwa marehemu, lakini alikuta chumba chake kimefungwa ambapo mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema kuwa, msiba ulihamishiwa Tazara-Mchicha kwa dada yake aitwae Doto ambaye ndiye pacha wake.
Mwandishi wetu alizungumza na majirani aliowakuta eneo hilo ambao walisema kuwa, kifo hicho kilisababisha mshtuko mkubwa mtaani hapo na kuibua majonzi makubwa.
Kutokana na afande huyo kuishi vizuri na majirani zake, mwandishi wetu aliwakuta wakiendelea kuchangisha pesa za rambirambi huku wakiwa na picha ya marehemu.
ACP Muliro Jumanne Muliro.
UJIJI, KIGOMA KWA MAZISHI
Mwanahabari wetu pia alifika alipoelekezwa ulipokuwa msiba huo, lakini alipofika alikuta tayari mwili wa marehemu ulishasafirishwa kupelekwa kijijini kwao, Ujiji mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.
MWANAJESHI MUHIMBILI
Habari kutoka Muhimbili zilidai kuwa mwanajeshi aliyepata kisanga hicho yeye anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo japokuwa hakuna afisa habari yeyote katika hospitali hiyo aliyekuwa tayari kuzungumzia tukio hilo.
“Ni kweli huyo mwanajeshi yupo, lakini chini ya ulinzi mkali, itakuwa vigumu ninyi kumuona,” alisema mmoja wa askari ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini hospitalini hapo.
KAMANDA MAMBOSASA
Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa alisema angempigia mwandishi baadaye.
KAMANDA MULIRO
Mwandishi aliamua kumpigia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Muliro Jumanne Muliro na alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema ni vema kuzungumza na Kamanda wa Kanda Maalum.
“Ndugu yangu si unajua kuwa kuna Kamanda wa Kanda Maalum? Mpigie yeye,” alisema Kamanda Muliro.
Alipoambiwa amepigiwa hajajibu swali ndiyo maana akapigiwa yeye RPC, Muliro alisema atampigia yeye Mambosasa.
Mwandishi alimpigia simu tena Kamanda Mambosasa na kumueleza kuhusiana na tukio hilo ndipo akasema yupo chumba cha daktari na akaahidi kumpigia mwandishi baadaye.
MSEMAJI WA POLISI
Hata hivyo, ili kupata undani wa tukio hilo, pia Uwazi lilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Barnabasi Mwakalukwa na kumuuliza juu ya taarifa za tukio hilo ambapo aliomba atafutwe Kamanda Mambosasa.
“Hilo jambo anayepaswa kulizungumzia ni Kamanda Mambosasa, mtafuteni huyo,” alisema Kamanda Mwakalukwa.
UWAZI LAMRUDIA MAMBOSASA
Uwazi lilimrudia tena Kamanda Mambosasa na kumtaka kulizungumzia tukio hilo ambapo alikiri na kusema kuwa, kulikuwa askari waliofanya tukio hilo walimdhania mwanajeshi huyo kuwa ni jambazi.
Haikujulikana mara moja kama polisi aliyempiga risasi mwenzake pamoja na mwanajeshi huyo kama amekamatwa au la.
KUMRADHI
Jina la Konstebo Justine Mtesigwa, ambalo awali lilitumika kwenye habari hii kwenye gazeti la Uwazi leo kwamba ndiye aliyeuawa lilikosewa, jina sahihi ya aliyeuawa ni konstebo Kulwa Gilbert. Justine na Kulwa walikuwa ni marafafiki na walikuwa wakifanyakazi pamoja Ukonga. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa Justine, ndugu, jamaa, marafiki na wafanayakazi wenzake – Mhariri.
Stori: Richard Bukos, Dar.
My Take;
Polisi wawili kupambana na Mwanajeshi mmoja asiye na silaha na kuishia kuuana wenyewe ni picha kuwa hawa wanahitaji mafunzo ya uhakika ili unyonge wao wasiutumie kuwaonea raia wasio hatia
HahahahhKwa hawa jamaa siwezi kusikitika kabisa na tena kama ingewezekana wangelipuana kikosi kwa kikosi
Akbadiri ALLAH AKBARKifo cha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Konstebo Kulwa Gilbert, aliyepigwa risasi kwa bahati mbaya na mwenzake, kimezua mshtuko kwa ndugu, jamaa, askari wenzake na majirani aliokuwa akiishi nao nyumbani kwake, Ukonga-Mazizini jijini Dar, Gazeti la Uwazi pekee ndilo lenye mkasa mzima wa tukio hilo.

Laan inawatafuna na mtamakizana wenyew Mungu si bashiteduuu, hapo ndo ujue kuwa weled ktk jeshi letu la polisi hamna kabisa, pia ata mwanajeshi hakuwa na hekima hata kidogo na anatakiwa kuadhibiwa vikali, haiwezekan umeshapewa tahadhali ya kutoka eneo hilo na unaona kabisa kitu kinachoendelea kwa mjibu wa sheria na kiusalama, halafu ww unadinda eti kisa ww ni mwanajeshi yaan alishindwa kutambua kwamba hapo kuna tukio linalohitaji usalama zaid, na alikosea zaid alipoishika silaha ya afande kama ni kweli, hapa polisi walitakiwa wamkamate kwa nguvu then wampe kichapo cha mbwamwitu ili ajue kuwa kaingia cha kike, askali aliyerusha risasi hakutumia weled wa kazi.
Ni ya kwakeHaya mambo ya kuleta ujuaji mwisho unaishia pabaya...huyo mjeda anajifanya mwamba usikute hapo atm alikuwa anatoa buku 10 tu
Kwani uliambiwa ni yako?Ni ya kwake
TPF iwekweli Tanzania Police Force sio CCM force. Operation regurations ziendane na matakwa ya Watanzania.Karma is a bit....ch
Jeshi la polisi lilifaa liundwe na wasome yaani wenye elimu ngazi ya degree na masters wenye G.P.A 2.5 kwasbb polisi ni msimamizi na muangalizi wa sheria.
Waliofeli form 4 walipaswa kwenda jeshi, na magereza. Km jeshi la polisi linageuzwa tawi la chama fulani. Unategemea nini kitatokea?
Jiulize km hapo. Mtu hana bunduki lkn unamtishia bunduki halafu cha kushangaza mwenzake analenga tu cha kushangaza hana hata shabaha.
Hapo kulikuwa hakuna haja ya kutumia silaha. Ni mazungumzo tu sbb wote wapo kwenye sekta moja lkn vitengo tofauti.
Kazi kweli kweli
Nilidhani umesema anaenda kumuhonga mamaako!Kwani uliambiwa ni yako?
Wangemwambia kwa lugha nzuri ingetokea nini hapo?Hapana, aliambiwa atoweke, yeye akadinda na kudai aambiwe "kistaarabu", Ndipo wakamuelekezea mtutu...