Bado huelewi.
Huwezi kujua kila kitu, unawezakujua mambo mengi sawa but huwezi kujua kila kitu.
Kule kwenye hivyo vyombo unavyosema wanachukua waliotaga kuna watu wa fani mbali mbali na elimu kubwa mpaka PhD unawakuta huko.
Elimu ndio huleta tofauti baina yao, lakini kazi ya kwanza ya Askari ni ulinzi, elimu ni nyongeza ya kukufanya ulipwe vizuri na ufanye kazi ya utaalam kuzido wenzako.
Sio kwamba ukiwa na Masters utapangwa kwenda ulinzi benki ukakataa, itabidi ukubali tu maana usipotii amri kijeshi unahesabika huna nidhamu.
Unajua majeshi yanaajiri wataalamu (wenye fani) wangapi kwa mwaka?
Wataalamu wa kule hawavai suti wala kuchomekea mashati ya kumeremeta ndio maana wewe unaona wote hawajasoma.
Nenda Jwtz uone watu walivyopiga shule
Nenda polisi uone watu walisoma
Nenda Magereza uone
Nenda uhamiaji
Nenda Fire.
Maisha ni tofauti na CV yako ya kukufanya uvae suti