Dar: Studio za Mjini FM zawaka moto huko Masaki

Dar: Studio za Mjini FM zawaka moto huko Masaki

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Studio za Mjini FM zimeteketea kwa moto asubuhi ya leo Januari 12, 2024 huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.

Video inamuonesha Dorah ambaye ni mmoja wa Watangazaji wa Mjini FM akiwa haamini kilichotokea leo Januari 12 2024.

Inspekta Kulwa Nzelekela kutoka jeshi ka uokoaji na zima moto kinondoni, Lugalo ameeleza madhara ambayo yamesababishwa na moto huo, huku jeshi hilo likiwa limefanikiwa kuudhibiti moto huo usiendelee kuathiri na maeneo mengine.

=====

Ajali ya Moto iliyotokea Studio za Mjini Fm Masaki Jijini Dar es Salaam leo asubuhi imeteketeza studio hiyo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni Lugalo, Inspecta Kulwa Nzerekera amethibitisha kutokea ajali hiyo waliyofanikiwa kuidhibiti, licha ya sehemu kubwa ya studio kutekekea kwa moto huo.



 
Back
Top Bottom