Dar to Kyela petrol lita ngapi?

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
1,595
Reaction score
3,416
kwa wazoefu naomba msaada,gari ya toyota noah old model(road tourer),kutoka dar mpaka kyela inaweza tumia litre ngapi za petrol?ni 1990cc, 2WD
 
Wewe jiandae na 250,000 one way mkuu...Mara ya mwisho kipindi hicho petrol ni 2630 trip ilikua hivi...140,000 full tank lita 53...Makambako...68,000 moro 35,000 tshs haya ndo yalifika mpaka Dar na kutumia kwa siku kadhaa...gari ina engine ya 3s..pia...
 
sijaelewa vizuri mkuu,ina maana toka kyela mpaka makambako ulitumia lita 53(140,000/),na makambako moro ulitumia ya 68000/(lita 26) na moro to dar sh 35000/(lita 13)?
 
umbali toka posta mpya dar mpaka kyela ni 925km,sasa sijui kwa injini ya 3s ya 1990cc,ulaji mafuta wake ni km ngapi kwa litre moja,na kwa speed gani?
 
sijaelewa vizuri mkuu,ina maana toka kyela mpaka makambako ulitumia lita 53(140,000/),na makambako moro ulitumia ya 68000/(lita 26) na moro to dar sh 35000/(lita 13)?
Hapana toka kyela nilijaza 140,000 ikawa full tank..nilipofika makambako nika top up 68,000 ili irudi kwenye full..nilipo fika moro nikaweka 35,000 ndo nikamaliza nayo hadi DSM kwaio dhumuni la kufanya hivyo ni kujua wese linaendaje nikakuta ni 10.32km/l kutoka Kyela hadi Mbeya kuna milima milima mingi kwaio kwa engine hio ya 3s hapo weka 250,000 mimi nakanyaga vibaya mafuta ila kama upo fresh unaweza tumia pungufu ya hapo kwaio around lita 83-85 unafika kyela mjomba
 
Ya nn kujitesa. Kwea New Force tu
asante kwa ushauri mkuu,ila safari sio mateso,unaweza ukifika iringa unalala siku moja,ukifika makambako unalala siku mbili,ni maamuzi tu mkuu,maisha yenyewe ni leo tu,kesho ni ya Mungu.
 
Mkuu kwa bei mpya ya mafuta dar na considering mafuta mengine utanunua kwa bei za huko mkoa ambazo ni juu kuliko dar, hapo 250,000 one way inahusika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…