Kwa mfano nimemsikia yule mwanaharakati wa Ubeligiji anasema anarudi nyumbani waje wajenge TANZANIA MPYA, yaani wajenge Tanzania ya kinadharia kwa sababu mm ninachojua haki za binadamu ni pamoja na kuwaheshimu na kuwalinda wamachinga, mamantilie, haki za binadamu ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya Reli, Anga,:majini na Nchi kavu, haki za binadamu ni pamoja na kulipa ada buree kwa watoto wa shule, haki za binadamu ni pamoja na kuimarisha ulinzi wa rasilimali za Taifa kama madini, haki za binadamu ni pamoja na kusaidia wajane watu waonewao, sasa hawa ndugu zangu wanaongea vitu too theoretical.