mpitanjia01
New Member
- Feb 13, 2023
- 2
- 3
Ni mwaka mmoja umepita hivi sasa, lakini hali ya barabara ya mtaa wa Chato inaleta utata kati ya wananchi na wakandarasi. Urefu wa barabara hii ni mita 600. Imekuwaje mpaka leo hii barabara haijakamilika? Ujenzi wa barabara hii ulianzishwa kwa nia ya kuweka bomba kuu la maji machafu chini. Ukiwa unapita Wakili House, utakuta bonge la shimo kwa nje ambalo linaangaliana na taasisi hii, na shule ya Primary ya Sunrise International School. Kinachotokea sasahivi ni kwamba, mvua yoyote ikinyesha, maji machafu hujikusanyika na kuleta mafuriko makubwa sana katika huu mtaa. Mafuriko haya yamearibu miundo mbinu, na mali za wakazi wa mtaa wa Chato.
Kuna vitu muhimu nataka kupoint, ili tuweze kujadiliana vizuri:
- Wakandarasi wameacha shimo la maji taka wazi, ambalo linaangaliana na Wakili House (Tanganyika Law Society) na Shule ya msingi ya Sunrise International School. Ki mazingira, NEMC wanalichukuaje hili swala?
- Kila wakati mvua zikinyesha, hutokea mafuriko ambayo yanahatarisha maisha ya wakazi na wapita njia. Je, mtoto wa Sunrise akisombwa na mafuriko, kuna hatua gani zitachukuliwa juu ya hili? Je, wazazi wa hawa watoto wanalichukuliaje hili swala?
- Ni nani anasimamia Uharibifu wa nyumba za wakazi wa mtaa wa Chato?
- Kwanini mamlaka za serikali wamekaa kimya?
- Nani anawasimamia wananchi wa Mtaa wa Chato?
- Baada ya ITV kurusha taarifa hii mwaka 2022, kwanini hakuna hatua zilizochukuliwa ?
- Ni kampuni gani inasimamia ujenzi huu?
- Je, TARURA wanachukuliaje hili swala?
- Je, itachukua muda gani hadi hii barabara ikamilike