Dar :Vijana 1,000 wachunguzwa, asilimia 80 wana shida ya afya ya akili

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Asilimia 80 ya vijana 1,000, wamebainika kuwa na changamoto za magonjwa ya akili bila kujua, imeelezwa.Kati ya hao, asilimia 20 wamewahi kujaribu kujiua, mkoani Dar es Salaam.Vilevile tatizo hilo limebainika kuwa pia kwa wazazi ambapo asilimia 90 ya wazazi 400, wamebainika kuishi na changamoto hizo, mkoani humo.

Changamoto za malezi, makuzi, migogoro ya familia, uchumi duni, uhasiano wenye migogoro na matatizo ya uzazi, ni mambo yaliyobainika kuwa yanachangia kwa ukubwa kuwa na changamoto pamoja na magonjwa ya akili.

Matokeo hayo yamebainika katika utafiti uliofanyika kwa siku 425 kupitia Mpango wa Afya Akili chini ya Taasisi ya SoJ ambao ulianza Agosti, 2025.

Mradi wa programu hiyo, Mtaalamu wa Tiba ya Saikolojia na Afya ya Akili, Dezidel Peter, alisema hayo jana akifafanua kuhusu suala hilo alipokuwa akizungumza na Nipashe kuhusu mwezi wa uhamasishaji kuhusu afya ya akili.

“Kila Jumamosi ya kila wiki, tunakutana na vijana au wazazi maeneo tofauti ya Dar es Salaam. Vijana hawa, asilimia kubwa ni wale wanaotoka katika mazingira magumu na kupewa misaada na vituo vya huduma ya kijamii na kijana vilivyo chini ya makanisa.

“Kupitia mradi wetu wa Afya ya Akili, tumekuwa tukikutana na vijana wenye umri wa miaka 12 na kuendelea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, tangu msimu wa kwanza hadi sasa tuko msimu wa pili. Tangu tumeanza programu sasa tuna mwaka mmoja na miezi minne.

“Katika mradi huo, hadi kupatikana kwa matokeo hayo, njia ya mazungumzo na mtu mmoja mmoja kwa nyakati tofauti tofauti pamoja na maswali kwa vikundi, vilitumika.“Upande wa vijana, tulianzisha msimu wa kwanza kwa wale walioruhusiwa na wazazi wao pamoja na ‘support group’ kwa wale wanaokuja kushiriki programu zetu. Upande wa wazazi tunawasaidia kupitia ‘support group’.

“Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba, bado unyanyapaa ni mkubwa, hivyo inatupa wakati mgumu sana. Bado programu zinaendelea, ndiyo kwanza tuko msimu wa pili, hivyo kuna misimu mingi inakuja na tunategemea kufikia Tanzania nzima,” alisema mtaalamu huyo.

Alisema mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa ni kuwafikia vijana zaidi ya 1,000 pamoja na wazazi zaidi ya 400 na changamoto kubwa walizozibaini ni zaidi ya asilimia 80 ya vijana wana changamoto za afya ya akili, lakini hawajui kama wana changamoto hizo na asilimia 90 ya wazazi wanaishi na changamoto ya afya ya akili,” alisema.

Peter alisema kwamba, kuna mambo muhimu yanayopaswa kutiliwa mkazo, kama vile elimu na uelewa kwa kutoa elimu ya kina ili kupunguza na hatimaye kuondoa unyanyapaa kuhusu afya ya akili.

Pia, alisema kuna haja ya kufikia jamii ya chini kwa kuhakikisha huduma na elimu inawafikia watu wa hali ya chini ambao mara nyingi hawasikiki na kushirikiana na viongozi wa dini.

“Watu wengi wenye changamoto za afya ya akili, huishi kwenye nyumba za ibada wakidhani wamepagawa na mapepo au wamerogwa, hivyo ushirikiano na viongozi wa dini ni muhimu sana kwa kutoa msaada wa matibabu kwa wenye changamoto na ugonjwa wa akili,” alisema.

Daktari wa Magonjwa na Afya ya Akili, Raymond Mgeni, alisema jamii inapaswa kuendelea kupewa elimu kwa kuwa historia inaonyesha jaribio la kukatisha uhai linaongeza nafasi za majaribio mengine baadaye.

“Shauku kubwa ni kusaidia jamii. Nakubaliana kabisa na suala la kushirikiana na taasisi za kidini linapokuja suala hili la afya ya akili na vijana,” alisema.

Chanzo: Habari Leo

UTAFITI.jpeg
​
 
Sasa mnategemea nini kama vijana wenyewendiyo wale wanao amini Mudi boy ni mtume mtakatifu au muhuni mwamposa
 
Hao wanaowapima wenzao, wao wamepimwa? Tuanzie hapo, usikute wenyewe ndio tatizo sugu.
 
Kuna kitu nashindwa kuelewa naonaga kila mtu ana changamoto za kimaisha kwa namna moja au nyingine zinaweza kumletea athali katika maisha ya kila mtu, sasa nashindwa kuelewa ni vigezo vipi wanatumia kupima kujua huyu ana changamoto na huyu hana.
 
Asilimia 80 ya vijana 1,000, wamebainika kuwa na changamoto za magonjwa ya akili bila kujua, imeelezwa.Kati ya hao, asilimia 20 wamewahi kujaribu kujiua, mkoani Dar es Salaam.Vilevile tatizo hilo limebainika kuwa pia kwa wazazi ambapo asilimia 90 ya wazazi 400, wamebainika kuishi na changamoto hizo, mkoani humo.

Changamoto za malezi, makuzi, migogoro ya familia, uchumi duni, uhasiano wenye migogoro na matatizo ya uzazi, ni mambo yaliyobainika kuwa yanachangia kwa ukubwa kuwa na changamoto pamoja na magonjwa ya akili.

Matokeo hayo yamebainika katika utafiti uliofanyika kwa siku 425 kupitia Mpango wa Afya Akili chini ya Taasisi ya SoJ ambao ulianza Agosti, 2025.

Mradi wa programu hiyo, Mtaalamu wa Tiba ya Saikolojia na Afya ya Akili, Dezidel Peter, alisema hayo jana akifafanua kuhusu suala hilo alipokuwa akizungumza na Nipashe kuhusu mwezi wa uhamasishaji kuhusu afya ya akili.

“Kila Jumamosi ya kila wiki, tunakutana na vijana au wazazi maeneo tofauti ya Dar es Salaam. Vijana hawa, asilimia kubwa ni wale wanaotoka katika mazingira magumu na kupewa misaada na vituo vya huduma ya kijamii na kijana vilivyo chini ya makanisa.

“Kupitia mradi wetu wa Afya ya Akili, tumekuwa tukikutana na vijana wenye umri wa miaka 12 na kuendelea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, tangu msimu wa kwanza hadi sasa tuko msimu wa pili. Tangu tumeanza programu sasa tuna mwaka mmoja na miezi minne.

“Katika mradi huo, hadi kupatikana kwa matokeo hayo, njia ya mazungumzo na mtu mmoja mmoja kwa nyakati tofauti tofauti pamoja na maswali kwa vikundi, vilitumika.“Upande wa vijana, tulianzisha msimu wa kwanza kwa wale walioruhusiwa na wazazi wao pamoja na ‘support group’ kwa wale wanaokuja kushiriki programu zetu. Upande wa wazazi tunawasaidia kupitia ‘support group’.

“Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba, bado unyanyapaa ni mkubwa, hivyo inatupa wakati mgumu sana. Bado programu zinaendelea, ndiyo kwanza tuko msimu wa pili, hivyo kuna misimu mingi inakuja na tunategemea kufikia Tanzania nzima,” alisema mtaalamu huyo.

Alisema mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa ni kuwafikia vijana zaidi ya 1,000 pamoja na wazazi zaidi ya 400 na changamoto kubwa walizozibaini ni zaidi ya asilimia 80 ya vijana wana changamoto za afya ya akili, lakini hawajui kama wana changamoto hizo na asilimia 90 ya wazazi wanaishi na changamoto ya afya ya akili,” alisema.

Peter alisema kwamba, kuna mambo muhimu yanayopaswa kutiliwa mkazo, kama vile elimu na uelewa kwa kutoa elimu ya kina ili kupunguza na hatimaye kuondoa unyanyapaa kuhusu afya ya akili.

Pia, alisema kuna haja ya kufikia jamii ya chini kwa kuhakikisha huduma na elimu inawafikia watu wa hali ya chini ambao mara nyingi hawasikiki na kushirikiana na viongozi wa dini.

“Watu wengi wenye changamoto za afya ya akili, huishi kwenye nyumba za ibada wakidhani wamepagawa na mapepo au wamerogwa, hivyo ushirikiano na viongozi wa dini ni muhimu sana kwa kutoa msaada wa matibabu kwa wenye changamoto na ugonjwa wa akili,” alisema.

Daktari wa Magonjwa na Afya ya Akili, Raymond Mgeni, alisema jamii inapaswa kuendelea kupewa elimu kwa kuwa historia inaonyesha jaribio la kukatisha uhai linaongeza nafasi za majaribio mengine baadaye.

“Shauku kubwa ni kusaidia jamii. Nakubaliana kabisa na suala la kushirikiana na taasisi za kidini linapokuja suala hili la afya ya akili na vijana,” alisema.

Chanzo: Habari Leo

Kamali.hizo
 
Utafiti fyongo kuwahi kufanyika kwenye nchi yetu. Yaani duniani yenyewe asilimia haiwezi kuwa kubwa kiasi icho usikute wafanya tafiti ni kina Kasheku Msukuma acheni kutishia watu
 
Back
Top Bottom