Dar: Wabunge 19 wa Viti Maalum waliovuliwa uwanachama na CHADEMA, Kuongea na Wanahabari

Status
Not open for further replies.
Hakuna msamaha kwa msaliti a.k.a uhaini. Imeisha hiyo
 
Pole Halima,

Dont regret much,

In life you try..

if you win,thats good,

You lose, You learn...

Good luck in your new adventure.
 
Mbowe anawafukuza ile sitaki nataka, kawaambia waombe msamaha watasamehewa. Fukuza gani halafu unamwambia omba radhi usamehewe?
 
Yaani na ule mzigo auachie..aaahh acha masihara..!!
Mzigo umeshaingia luba kaka. Bora aombe msamaha na atasamehewa. Halima bado kijana sana hivyo bado ana safari ndefu sana ya kisiasa. Akishupaza shingo anaenda kupotea mazima kwenye siasa.
 
Waanze kuomba radhi Mnyika kwa kupeleka majina 30 tume
 
Bado kilichotokea ni kizungumkuti na picha haijaeleweka bado.
Tunajua palikuwa na mvutano kuhusu kupeleka au kutopeleka majina na wadadisi wa mambo na wapiga ramli wakatueleza ya kuwa kuna mawasiliano kati ya Mashinji na Bulaya.
Bulaya akajibu kuwa msimamo wake kwa Chama hauyumbi.
Kwa upande mwingine Nusrat na Twaha wamesota rumande miezi minne ghafla Nusrat anatolewa usiku na kuapishwa kesho yake.
Huku tunashuhudia kuapishwa nje ya utaratibu tuliozoea na kwa siasa za sasa tlitegemea hawa wasindikizwe kwa kila aina ya chereko kama jibu kwa Chadema lakini haikuwa hivyo.Je,
  1. Ni kweli Ndugai alipokea majina toka NEC?
  2. Je ni kweli waliomtoa Nusrat usiku na kumwapisha kesho yake walikuwa hawajui kuwa linaweza kuhojiwa?
  3. Je Nusrat kwa adha na tabu aliyopata alikuwa laini haraka kiasi hiki kwa sababu gani?
Binafsi nahisi kuna aina ya vitisho au ulaghai mkubwa uliofanyika.
Naungana nawe of all people Halima jivue ubunge bandia,omba msamaha Chadema.Nafsi yako itapata amani kubwa.
Pia nahisi kuna mahali watu wanatii amri bila kutafakari na mwisho wa yote wansababisha aibu.
 
Hivi unaweza kumshauri mtu mzima jambo simple kama hilo ? Kwa hiyo unafikiri mpaka leo hii Halima Mdee hajui anataka nini na maisha yake ?
 
Mzigo umeshaingia luba kaka. Bora aombe msamaha na atasamehewa. Halima bado kijana sana hivyo bado ana safari ndefu sana ya kisiasa. Akishupaza shingo anaenda kupotea mazima kwenye siasa.

Kila mtu ana malengo yake,huwezi jua kwamba baada ya 15 years ndani ya siasa/Chadema labda kwake safari yake kisiasa anaweza kufikiria imefikia kikomo..so she has nothing to lose,labda km angekuwa na 1-5 years kny game la siasa ungesema 'kijana'
 
Hata Mimi namshauri kuwa aombe radhi naamini atasamehewa tu. Maana kila binadamu ana mapungufu yake.
 
Wazungu wanasema the damage is done pamoja na kwamba mnaona kama hakuna kilicho haribika, CDM inaelekea njia ya CUF, Lissu katimua, Lema katimua, Halima na Bulaya wameona bora na wao wakajitafutie maisha kimpango wao. Wa maana alie baki CDM ni mbowe peke yake. Ruzuku ndio imepotea, magu amebana kila kona kwaiyo wafadhili hela hamna.
 

Mwanamke ndiye chanzo kikuu cha usaliti duniani.
 
Busara za kawaida zinamtaka Mdee na genge lake kwa sasa wachutame wasubiri muda kidogo upite then wawaombe msamaha Chadema na Watanzania kwa ujumla
Bila shaka walitegemea hii reaction kutoka CHADEMA. Hapa options zao zipo limited na ya haraka kwao ni kukimbilia mahakamani tu na hao waliowatuma wanaweza kuwasaidia japo kwa muda flani.

Kamati Kuu kimsingi imefanya maamuzi sahihi. They had no other option.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…