Dar: Wabunge waipongeza TRA kufungua ofisi ya walipa kodi binafsi wenye hadhi ya juu

Dar: Wabunge waipongeza TRA kufungua ofisi ya walipa kodi binafsi wenye hadhi ya juu

TRA Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
128
Reaction score
370
cg na wabunge ltd 3.jpg

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuanzisha Ofisi ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu hali ambayo itaongeza ufanisi katika kuhudumia kundi hilo ambalo ni wachangiaji wakubwa wa mapato ya TRA.

Wakiwa katika ziara ya kutembelea Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu kwa nyakati tofauti Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wamepongeza ubunifu uliofanywa na Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda kwa kuanzisha Ofisi hiyo ambayo ina hadhi inayotakiwa.

"Ubuni huu ni wa kipekee kabisa na unaweza usiamini kama Serikali inaweza kuwa na Ofisi zenye hadhi kiasi hiki, hata Walipa Kodi wenye hadhi ya juu wakija kuhudumiwa wataona wamethaminiwa" wamesema baadhi ya Wabunge wakati wa ziara hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Oran Njeza amesema Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu wakithaminiwa hata mapato ya TRA yataongezeka zaidi maana watalipa Kodi kwa hiari na kujenga urafiki na TRA.

Mhe. Njeza amesema Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu wanapopewa hadhi wanayostahili wanajisikia kuwa kulipa Kodi ni haki yao maana wanapata huduma zinazowastajili.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Mwenda amesema lengo la kuanzisha Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu ni kutaka kuwapa huduma inayolingana na hadhi yao.

Amesema Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu ina watumishi wabobezi katika masuala ya Kodi na huduma kwa wateja, huku kukiwa na mazingira mazuri ya kutolea huduma yenye hadhi ya juu.

cg na wabunge ltd 2.jpg
 
Hiyo pesa makapuku wengi wamewekeza na wanaizungusha. Sidhani kama ofisi nzuri au faragha ndio zinafanya watu walipe kodi bali ni sera na sheria rafiki za kodi.
Hiyo ni KODI inayoenda TRA sio MTAJI wa kuwekeza.

Yani TRA kodi uwe unaenda peleka kuanzia B kwenda mbele, maana yake utakua umewekeza mtaji mara dufu wa kukupa hiyo 1B ya kupeleka TRA.
 
Mngefafanua hao wa hadhi ya juu sifa zao ni zipi? Vipi mmefikiria na wachangiaji wakubwa wa PAYE?
Unataka Ujue ili uone kama nawewe unastahili kwenda pale?

Pale ni V.V.V.I.P haswa, pale ndio ukitulia getini utawaona wenye nchi yao wakiingia na kutoka.

Ukiona Mtu karidhia kwa MOYO wake wote kulipa kodi 1B kwenda Mbele ujue huyo sio mwenzetu.
 
Hiyo ni KODI inayoenda TRA sio MTAJI wa kuwekeza.

Yani TRA kodi uwe unaenda peleka kuanzia B kwenda mbele, maana yake utakua umewekeza mtaji mara dufu wa kukupa hiyo 1B ya kupeleka TRA.
Sawa hao watu wapo wengi, kwahiyo wawe wanatoka mikoani kwenda kwenye ofisi nzuri dar. Hivi hawa wadogo nao wakisusa wanataka ofisi nzuri, unadhani TRA watakusanya kodi nyingi kutoka kwa hao wenye misamaha lukuki na wakwepa kodi wakubwa.

Na bunge linabaki kupongeza matabaka yanavyojengwa. Mimi naungana na mdau hapo kwenye comment ya kwanza, ni faragha kwaajili ya kupeana rushwa.
 
Unataka Ujue ili uone kama nawewe unastahili kwenda pale?

Pale ni V.V.V.I.P haswa, pale ndio ukitulia getini utawaona wenye nchi yao wakiingia na kutoka.

Ukiona Mtu karidhia kwa MOYO wake wote kulipa kodi 1B kwenda Mbele ujue huyo sio mwenzetu.
Wenye investment zenye NP ya ku declare 3B huwa hawaend TRA mkuu...

TRA tunaenda sisi kupigishana kelele za Lak nne tano..
 
Kwa anaefahamu, walipa kodi hao ni wawekezaji wenye mtaji kuanzia kiasi gani?
Asante kwa swali zuri:

Ofisi hii itahusika zaidi na
1: Wakurugenzi wa makampuni yenye Mauzo ghafi (turn over)ya kuanzia Shilingi za kitanzania 20B kwa mwaka
2: Wenye biashara ya kushirikiana (partnership) zenye mauzo ghafi ( turnover)ya kuanzia shilingi za kitanzania 20B
3: Watu binafsi wenye hisa kwenye kampuni zilizowekeza Soko la Hisa la Dar e salaam (DSE)yenyye thamani ya uwekezaji kuanzia 2.5B
 
Nilikua nafanyia kampuni x. Ilikua ikifikia karibu na tarehe za kufile tunapigiwa simu na kuulizwa tuna tuna expect kufile kiasi gani.
 
Asante kwa swali zuri:

Ofisi hii itahusika zaidi na
1: Wakurugenzi wa makampuni yenye Mauzo ghafi (turn over)ya kuanzia Shilingi za kitanzania 20B kwa mwaka
2: Wenye biashara ya kushirikiana (partnership) zenye mauzo ghafi ( turnover)ya kuanzia shilingi za kitanzania 20B
3: Watu binafsi wenye hisa kwenye kampuni zilizowekeza Soko la Hisa la Dar e salaam (DSE)yenyye thamani ya uwekezaji kuanzia 2.5B
Hopeless, kama hao ni wathamani mbona mnashinda kukamata kamata hawa wa chini kana kwamba mkizikosa pesa zao mnafirisika wakati mnao hao mnaowajengea na ofisi binafsi. Mkitaka watu walipe kodi wekeni mazingira rafiki kama vile sera, sheria za kodi nzuri n.k, haya mnayofanya sasa ni ufisadi ni aidha mchinjwe Christmas au mfungwe jela.
 
Officers wa TRA baadhi yao ambao ni wengi wanachowaza ni kutengeneza mazingira ya Rushwa pekee na sio utendaji wa kazi.. kitu kizuri kuhusu rushwa ni Win win situation to both side
 
Back
Top Bottom