Dar: Wabunge waipongeza TRA kufungua ofisi ya walipa kodi binafsi wenye hadhi ya juu

Dar: Wabunge waipongeza TRA kufungua ofisi ya walipa kodi binafsi wenye hadhi ya juu

Asante kwa swali zuri:

Ofisi hii itahusika zaidi na
1: Wakurugenzi wa makampuni yenye Mauzo ghafi (turn over)ya kuanzia Shilingi za kitanzania 20B kwa mwaka
2: Wenye biashara ya kushirikiana (partnership) zenye mauzo ghafi ( turnover)ya kuanzia shilingi za kitanzania 20B
3: Watu binafsi wenye hisa kwenye kampuni zilizowekeza Soko la Hisa la Dar e salaam (DSE)yenyye thamani ya uwekezaji kuanzia 2.5B
Hio ni kweli kwa HNWIs bil 20 , japo wapo wanaouza hio hela ila kutokana na biashara zao hawatoi risiti ipasavyo na hawatakuja huko.

Shusheni hata bilioni 10 au muweke class (HNWNs, Prestige HNWIs na royal HNWIs)ya kituo lets say kuna ofisi ya wenye revenue ya bil 8-10 kuna 10-20 na over 20 bilion maana kuna wanao uza bil 20 ila margin 5% ,kuna wanaouza bilioni 10 ila margin 25%

Nimewaza bila kufikiria ,asante
 
Sawa hao watu wapo wengi, kwahiyo wawe wanatoka mikoani kwenda kwenye ofisi nzuri dar. Hivi hawa wadogo nao wakisusa wanataka ofisi nzuri, unadhani TRA watakusanya kodi nyingi kutoka kwa hao wenye misamaha lukuki na wakwepa kodi wakubwa.

Na bunge linabaki kupongeza matabaka yanavyojengwa. Mimi naungana na mdau hapo kwenye comment ya kwanza, ni faragha kwaajili ya kupeana rushwa.
Nakubaliana nawewe eneo 1 la "matabaka" sisi wote ni walipa kodi kila mtu kulingana na biashara anayofanya.

Mimi ni Mteja Mkubwa sana kulingana na Biashara yangu, Wewe kadhalika kila mtu na Engo yake ya biashara.

Hii kusema hawa wakubwa na hawa wadogo ni kuwadharau wananchi wazi wazi.
 
Maboresho haya yangezingatia OFISI zote za TRA ziwe na muonekano na hadhi ya kisasa sababu kila mlipa kodi ni mtu wa thamani na wa muhimu.

Kuwa na biashara kubwa hakufanyi umdharau mwenye biashara ndogo.

Nakubali DUNIANI hamna uSAWA ila kasoro ndogi ndogo kama hizi zifanywe na watu binafsi na sio SERIKALI.

Wananchi wote ni wa Serikali wana haki sawa bila kujali kipato/dini/kabila.

UChezeaji wa PESA za wananchi tu, maana hata hao WALIPA KODI WAKUBWA pesa zao zinajenga bara bara zinazotembelewa na boda boda na watembea kwa miguu.

Kodi zao sio kwamba zinatengwa zinafanyia JAMBO tofauti na sisi wadogo, KODI zote zinakusanywa zinaenda Fanya jambo la pamoja.

Na matokea tunasema SERIKALI imefanya na wala si WALIPA KODI WAKUBWA.

HII KITU haijakaa sawa nadhani ni matokeo ya udhaifu wa uwezo wa kufikiri wa viongozi waliopo katika maamuzi.

Halafu unaona kabisa kuna majibunya NDIO NDIO NDIO kwa kila wazo linaloletwa.

Hii ni MBAYA.
 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuanzisha Ofisi ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu hali ambayo itaongeza ufanisi katika kuhudumia kundi hilo ambalo ni wachangiaji wakubwa wa mapato ya TRA.

Wakiwa katika ziara ya kutembelea Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu kwa nyakati tofauti Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wamepongeza ubunifu uliofanywa na Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda kwa kuanzisha Ofisi hiyo ambayo ina hadhi inayotakiwa.

"Ubuni huu ni wa kipekee kabisa na unaweza usiamini kama Serikali inaweza kuwa na Ofisi zenye hadhi kiasi hiki, hata Walipa Kodi wenye hadhi ya juu wakija kuhudumiwa wataona wamethaminiwa" wamesema baadhi ya Wabunge wakati wa ziara hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Oran Njeza amesema Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu wakithaminiwa hata mapato ya TRA yataongezeka zaidi maana watalipa Kodi kwa hiari na kujenga urafiki na TRA.

Mhe. Njeza amesema Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu wanapopewa hadhi wanayostahili wanajisikia kuwa kulipa Kodi ni haki yao maana wanapata huduma zinazowastajili.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Mwenda amesema lengo la kuanzisha Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu ni kutaka kuwapa huduma inayolingana na hadhi yao.

Amesema Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu ina watumishi wabobezi katika masuala ya Kodi na huduma kwa wateja, huku kukiwa na mazingira mazuri ya kutolea huduma yenye hadhi ya juu.

Yaani TRA bhana hapo kuna ubunifu gani sasa! Wameshindwa kuwahudumia kwa ujumla saizi wameamua kuwatenga ili wajipakulie minyama.
 
Unataka Ujue ili uone kama nawewe unastahili kwenda pale?

Pale ni V.V.V.I.P haswa, pale ndio ukitulia getini utawaona wenye nchi yao wakiingia na kutoka.

Ukiona Mtu karidhia kwa MOYO wake wote kulipa kodi 1B kwenda Mbele ujue huyo sio mwenzetu.
Wenye kulipa Kodi kubwa hivyo huwezi wakuta kwny hio ofisi.Hapo utawaona wafanyakazi wa KPMG,EY,DELLOITTE&TOUCHE ,PWC
 
Back
Top Bottom