DAR: Wafanyabiashara Wakamatwa na Lita 5,000 za Oil Bandia

DAR: Wafanyabiashara Wakamatwa na Lita 5,000 za Oil Bandia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amethibitisha kukamatwa kwa Wafanyabiashara wawili wakiwa na galoni zaidi elfu tano (5000) za oil feki Jijini Dar es salaam kufuatia taarifa za uwepo wa Mtandao wa Wafanyabiashara wanaozalisha na usambazaji wa vilainishi (Oil) bandia ambazo zimekuwa zikifungashwa upya kwa kutumia nembo maarufu kama ya TotalEnergies.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Aprili 7, Waziri Kapinga amesema operesheni hiyo ilifanywa na FCC February 2026 katika eneo la Kariakoo ambapo Wahukiwa Wafanyabiashara hao wawili walikuwa wakitumia pia lebo bandia katika ufungashaji.

"Hapa kuna aina mbili, kuna wale ambao wanachukua ile ambayo ni OG wanajaza kwenye chupa ndogondogo, alafu kuna wale ambao sasa ni oili chafu wanachukua zile package za oili ambazo zimeshatumika wanajaza upya kwa ile oili chafu ndio hizi elfu tano ambazo tunazizungumzia, tunawashukuru sana FCC na wengine" - Waziri Judith Kapinga.

 
Unakuta chombo inafika Moshi na unajiaminisha umeweoa total oil kumbe ni takataka tu
 
Hawa wapumbavu siyo wa kuwachekea hata kidogo.

Unanunua oil ya Total Energies, kitu kinasoma Quartz nini sijui 50 40...! Unaendesha kilomita zisizozidi 1000, unapima oil unakutana na maji tu.
 
Back
Top Bottom