Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akibainisha hayo Machi 1, 2025, Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Kinondoni, Lilian Mwombeki amesema wamefanya zoezi la kawaida la ukaguzi wa kushtukiza kulingana na Sheria ya Vipimo Sura Namba 340 pamoja na mapitio yake ya Mwaka 2002 na kubaini changamoto za baadhi ya Watu ambao si waadilifu kutumia mizani isiyo kuwa na sifa kutoa huduma kwa Wananchi.
Aidha, Meneja huyo ameeleza waliponunua bidhaa hiyo kwenye bucha la pili kwa kiasi cha kilo 2 ikaleta Gramu 1,600 badala ya Gramu 2,000 ambapo ilionekana imepunjwa kwa Gramu 400 hii imeonekana kwamba mizani mingi huwa haizingatii uhalali wa vipimo kwa wateja ambao ndio watumiaji wa bidhaa hiyo.
Imeelezwa wahusika wanaoidaiwa kukiuka Sheria za vipimo kwa makusudi wanashitakiwa kwa kulipishwa faini au kupelekwa Mahakamani.
Pia soma:
~ Wafanyabiashara wa bucha sio waaminifu kabisa hasa wa Mbezi kwa Msuguri, wanaibia wateja
~ Wauzaji wa nyama Mbezi Beach kuna michezo wanafanya kwenye mizani
~ Waziri Jafo: Wauza nyama Buchani kuna ujanjaujanja wanaufanya kuibia Wateja kwenye mizani