Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,427
Waliokamatwa ni wafanyakazi wa Kampuni ya Ukandarasi ya CHICCO pamoja na Kampuni ya Ukandarasi ya Nyanza.
Kampuni ya Chicco inatekeleza miradi ya ujenzi Mto Sinza hadi Mto Ng’ombe huku Kampuni ya Nyanza Road Works ikishika tenda za ujenzi wa barabara za Banana, Kivule na Kitunda
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Katibu Tawala Mkoa, Abubakar Kunenge amesema kuwa Serikali imewekeza kiasi cha bilioni 32.
Ameeleza kuwa tayari Mkandarasi amekwishalipwa Bilioni 4.8 lakini bado wanafanya kazi chini ya kiwango
Kampuni ya Nyanza Road Works yenyewe tayari imeshalipwa kiasi cha Shilingi milioni 877 sawa na 15% lakini Daraja la alilolijenga katika mradi wa barabara ya Kivule limeleta maafa.
Hivyo kwa kutumia vifungu 7 na 2 na 15 kidogo cha pili cha sheria tawala za mkoa Mkuu wa Mkoa ameagiza wakamatwe na kuwekwa ndani.
Kunenge ameongeza kuwa Wakandarasi wote waliopewa zabuni mbalimbali ndani ya Jiji la Dar Es Salaam na wakiona kuwa hawawezi kutekeleza miradi kwa uhakika basi wajiondoe wenyewe.