Dar: Wafariki baada ya kuangukiwa na kifusi Kigamboni leo Aprili 3, 2022

Dar: Wafariki baada ya kuangukiwa na kifusi Kigamboni leo Aprili 3, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Watu kadhaaa wanahofiwa kufariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakiwa kwenye shughuli za machimbo ya mawe katika eneo la machimbo ya Kikikaka, Mji Mwema Kigamboni, Dar es salaam. Kwa mujibu wa taarifa za awali shughuli za uokoaji zinaendelea.

Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio inadaiwa kuna watu watatu wamepoteza maisha na tayari miili yao imeshatolewa, bado mamlaka za usalama hazijatoa tamko juu ya uthibitisho huo.

Kifusi Kigamboni.jpg


277819959_538064737880019_7179022972085506849_n.jpg


Picha: Millard Ayo
 
Duh...

Hiyo picha ndo harakati zinaendelea.....!!!😟😟😟

Ikiwa na mtu anayekuhusu ni maumivu mara mbili.
 
Dar es Salaam. Watu watatu wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika machimbo ya kikikaka, Mjimwema - Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kudondokewa na kifusi wakati wakipakia kokoto katika gari.

Tukio hilo limetokea leo Aprili 3, 2022 saa saa tatu asubuhi katika machimbo hayo ambayo awali yalikuwa yakitumiwa na wachimba kokoto wadogo kabla ya Serikali kuyafunga mwaka 2018.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa amesema baada ya taarifa za tukio, jitihada za uokoaji zilianza.

"Mwanzoni tulikuwa hatuna idadi kamili kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa na uwezo wa kuthibitisha kuna watu wangapi huko chini, lakini tulipoongea na viongozi wa maeneo haya walituambia kuwa siku za mwisho wa wiki huwa hazina watu wengi.

"Jitihada zimefanyika za uokoaji na tumefanikiwa kutoa kifusi hadi kugusa mwamba na kutoa miili mitatu ya jinsia ya kiume na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Vijibweni” amesema Fatma

Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa maeneo hayo kuwa yeyote ambaye atakuwa na taarifa au kutomuona ndugu yake na anafanya kazi katika machimbo hayo atoe taarifa ili hatua nyingine za ufuatiliaji zichukuliwe.
 
Back
Top Bottom