Dar: Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope, watakiwa kuhama

Dar: Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope, watakiwa kuhama

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


RC KUNENGE AWAELEKEZA WAKAZI WA KUNDUCHI MTONGANI AMBAO NYUMBA ZAO ZIMEHARIBIWA NA "VOLCANO YA TOPE" LINALOTOKA ARDHINI KUHAMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewaelekeza baadhi ya Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope linalofuka kutoka ardhini kuhama Mara moja ili kujikinga na maafa wakati Serikali inaendelea kufanya utafiti wa kujua ukubwa wa eneo lililoathirika.

Mapema leo RC Kunenge akiongozana na wajumbe wa kamati ya usalama ya Mkoa wamefika Katika eneo hilo na kushuhudia uwepo tope linalotoka ardhini na kupanda Katika uso wa ardhi jambo lililosababisha baadhi ya nyumba kutitia, kupasuka nyufa na mifugo kutitia jambo lililosababisha taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo RC Kunenge amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuweka alama za hatari Katika eneo hilo wakati Serikali chini ya taasisi ya Geologia na utafiti wa Madini Tanzania ukiendelea kupia ukubwa wa eneo lililoathirika.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Serikali inaangalia utaratibu wa kuwapatia wananchi wa eneo hilo Viwanja vingine ili waweze kuendelea na maisha kama awali.

Kwa upande wake Mtafiti kutoka taasisi ya Geologia na utafiti wa Madini Bwana Gabriel Mbogoni amesema matokeo awali wamebaini chanzo Cha tope hilo ni mgandamizo uliosababishwa na uwiano wa maji na chembechembe za udongo kuharibika na kusababisha tope ambalo linasukumwa kutoka chini kwenda kwenye uso wa ardhi.

Aidha Bwana Mbogoni amesisitiza kuwa tope hilo wamelipima na kukuta likiwa na joto la kawaida hivyo halina uhusiano wowote na ile volcano inayorusha majivu na Moto utokanao na miamba iliyoiva hivyo eneo hilo kwa Sasa ni tete na halifai kwa shughuli za Ujenzi Wala makazi.
IMG-20201122-WA0024.jpg
IMG-20201122-WA0025.jpg
IMG-20201122-WA0026.jpg
IMG-20201122-WA0027.jpg
 
Picha mkuu wengine tupo mkoani huku hatujaona huo mtitio.
 
Kweli Tanzania nchi ya ki-communist, yaani Viwanja vyote ni mali ya Serikali ? Serikali inaamua tu kutoa viwanja kama sadaka na siyo kununua ? Bila ya kubadilisha huu mfumo (kwa uangalifu mkubwa lakini) kuendelea ni ngumu sana, binafsi siwezi kuwekeza mabilioni kama ninayo kama siwezi kumiliki chochote, hilo eneo sio mali yangu ndiyo maana yake, nchi za ki-capitalist unamiliki ardhi mpaka hata chote kilicho chini ya ardhi yako, kama madini au mafuta ni yako maadamu kiwanja ni chako.

Long Live Capitalism !
 
Kweli Tanzania nchi ya ki-communist, yaani Viwanja vyote ni mali ya Serikali ? Serikali inaamua tu kutoa viwanja kama sadaka na siyo kununua ? Bila ya kubadilisha huu mfumo (kwa uangalifu mkubwa lakini) kuendelea ni ngumu sana, binafsi siwezi kuwekeza mabilioni kama ninayo kama siwezi kumiliki chochote, hilo sio mali yangu ndiyo maana yake, ...
Umeanza kua mpinzani?
 
Dar kulivyo tambarare kunatokea volcano? Ama kweli serikali ya awamu hii inachapa kazi.
 
Baada ya miaka ya nyuma kabisa eneo la Kawe kusifika kuwa na Uchawi kuna Mtu pia aliwahi kuniambia sasa umehamia mno Kunduchi Mtongani.
 
Kweli Tanzania nchi ya ki-communist, yaani Viwanja vyote ni mali ya Serikali ? Serikali inaamua tu kutoa viwanja kama sadaka na siyo kununua ? Bila ya kubadilisha huu mfumo (kwa uangalifu mkubwa lakini) kuendelea ni ngumu sana, binafsi siwezi kuwekeza mabilioni kama ninayo kama siwezi kumiliki chochote, hilo eneo sio mali yangu ndiyo maana yake, nchi za ki-capitalist unamiliki ardhi mpaka hata chote kilicho chini ya ardhi yako, kama madini au mafuta ni yako maadamu kiwanja ni chako.

Long Live Capitalism !
Ardhi iendelee kuwa chini ya serikali hivyohivyo
 
Hi ndio tofauti kubw kati ya Makonda na Kunenge.

Kama ingelikua ni Makonda, I'm sure hili tukio lingekau considered kama maafa. Na bilashaka waathirika wange hamishwa na kuandaliwa makazi mapya.

Yaani sijui Makonda alikua anatoa wapi pesa, and he was very active.
 
Back
Top Bottom